Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

© UNICEF/Karin Schermbrucke

Juhudi za wakunga na wauguzi kuhudumia jamii wilaya ya Pangani, Tanzania

Mwaka wa 2020 ni mwaka wa kutambua mchango wa wauguzi na wakunga katika kufanikisha afya kwa wote. Nchi mbalimbali kwa kutambua mchango wa watu hawa, zimechukua hatua kuwawezesha licha ya kwamba bado idadi ya wauguzi kwa wagonjwa katika nchi nyingi haijafikia viwango vinavyohitajika.

Tanzania ni moja ya nchi ambazo zinaendelea kuweka msistizo katika kuimarisha idadi ya wauguzi kwenye hospitali. Katika Makala hii, Saa Zumo wa radio washirika amevinjari hospitali ya Pangani na haya ni mahojiano yake na mgeni wa leo anaanza kwa kujitambulisha

Sauti
4'59"
© UNICEF

Ukunga na uuguzi ni wito- Bwana Abdalla

Wakati dunia ikiadhimisha mwaka wa wakunga na wauguzi kutokana na mchango wa wahudumu  hao wa afya, shirika la afya ulimwenguni, WHO limesema sekta ya afya inahitaji huduma zaidi ya kundi hilo kwa kuwa wana mchango mkubwa katika kufanikisha huduma za afya na hivyo kufikia malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, hususan lile namba 4 la afya na ustawi.

Sauti
4'3"
UNFPA Mozambique

Nilivutiwa kuwa muuguzi kwa sababu mama yangu alikuwa muuguzi-Jackline Ayuma

Wakati dunia ikiadhimisha mwaka wa wakunga na wauguzi, shirika la afya ulimwenguni limesema nguvu kazi thabiti ya kundi hilo ni muhimu katika kufikia afya kwa wote.

Hatahivyo, WHO imesema mara nyingi wauguzi na wakunga hawathaminiwi na hushindwa kufikia uwezo wao kamili. Mwaka 2020 tunalenga kuhakikisha kwamba wauguzi na wakunga wanafanya kazi katika mazingira ambayo ni salama, wanakoheshimiwa na wafanyakazi wenzao na wanajamii na kwmaba wanafikia huduma ya afya na wanakofanyia kazi wanajumuishwa na wataalam tofauti wa kiafya.

Sauti
2'41"
UNFPA

Wauguzi waleta nuru katika kinga dhidi ya magonjwa, Uganda

Wakunga na wauguzi ni muhimu sana katika masuala ya uhamasishaji kuhusu masuala ya afya na hatimaye kuimarisha kinga badala ya kuponya.

Nchini Uganda has amafharibi mwa nchi, wauguzi na wakunga wanasifiwa kwa mchango wao katika uelimishaji wa jamii kuhusu afya ambao umesaidia kupunguza milipuko ya magonjwa hususani surua.

Ili kufahamu kwa undani, hii hapa majojiano kati ya John Kibego na Katibu wa masuala ya afya wa almashauri ya wilaya ya Hoima Jackson Mugenyi Mulindamburra amabye pia ni miongoni mwa waliochagiza uanzilishi wa chuo cha wauguzi na wakunga mjini Hoima.

Sauti
3'35"
UNICEF/UN0159224/Naftalin

Hatuna namna ya kupunguza vifo vya watoto wachanga na wazazi  tukiwaweka pembeni wauguzi wakunga- Amir Batenga

Kupitia mfululizo wa makala za Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa ambazo zinaangazia wakunga na wauguzi katika mwaka huu wa 2020 ambao umetambuliwa na Umoja wa Mataifa kama mwaka wa kuwaenzi wauguzi na wakunga, Amir Batenga wa UNFPA Simiyu akitekeleza mradi wa kusaidia kupunguza vifo vya watoto wachanga na wanawake, mkoani Simiyu Tanzania  kupitia makala hii anamweleza Stella Vuzo wa Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa, Dar es Salaam nchini Tanzania namna ambavyo UNFPA imesaidia kuokoa maisha ya akina mama na watoto wachanga kutokana na ushirikiano na wauguzi na wakunga.

Sauti
3'29"
UN

UNFPA na harakati zake za kuhakikisha huduma ya afya ya uzazi kambini

Wakati mkimbizi anajikuta ukimbizini, mahitaji yake yanakuwa ni mengi lakini kwa mazingira aliyonayo anajikuta akitegemea msaada wa kibinadamu kutoka mashirika. Mara nyingi hutokea kwamba mahitaji ambayo yanapewa kipaumbele ni yale ya msingi ikiwemo maji, chakula na huduma za kujisafi. Hata hivyo huduma ya afya na hususan afya ya uzazi inakuwa ni moja ya mahitaji muhimu hususan kwa mama na mtoto.

Sauti
6'25"
UNICEF/UN0159224/Naftalin

UNFPA imesaidia sana kuboresha huduma za afya ya uzazi visiwani Zanzibar- Azzah Amin Nofli

Kupitia mfululizo wa makala za Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa ambazo zinaangazia wakunga na wauguzi katika mwaka huu wa 2020 ambao umetambuliwa na Umoja wa Mataifa kama mwaka wa kuwaenzi wauguzi na wakunga, Azzah Amin Nofli Afisa programu wa afya ya uzazi, Ofisi ndogo wa shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia idadi ya watu, ofisi ndogo ya Zanzibar.

Sauti
3'55"
UNICEF/UMichele Sibiloni

Pesa ni muhimu, lakini kwangu mimi, muhimu zaidi ni afya ya mtu- Francis Maina

Kijana Francis Maina ni mwanafunzi wa Chuo cha uuguzi cha St. Regina kilichoko maeneo ya magharibi mwa nchi ya Uganda. Kijana huyu anasema kuwa pamoja na kwamba anasomea kazi ambayo mara nyingi malipo yake ni kidogo, yeye yuko tayari kuifanya kazi hiyo katika hali yoyote kwani furaha yake ni kuona mgonjwa wake akipata huduma nzuri na kisha suala la maslahi litafuata baadaye.

Sauti
3'33"
© UNICEF/Thomas Nybo

Jamii ya sasa wana imani zaidi na hospital kuliko wakunga wa jadi-Mkunga wa jadi

Kwa miaka mingi kabla ya ukuaji wa teknolojia na hata baada ya kuanzishwa hospitali za kisasa, jamii nyingi ziliendelea kuwatumia wakunga wa jadi kuwasaidia akina mama wajawazito kujifungua hususani kwa wale walikuwa mbali na huduma za kiafya. Bi Rehema Muhando wa kijiji cha Mwera huko Pangani Tanga Tanzania anasema ameifanya kazi ya ukunga kwa miaka mingi na anajivunia kuwa watoto wengi wamepita mikononi mwake. Lakini anasema hivi sasa, jamii imebadilika sana. 

Sauti
6'5"
UN /MINUSCA

Jamii yetu imenufaika sana na matangazo ya redio za kijamii.

Ikiwa leo ni siku ya redio duniani ambapo ulimwengu unakiangazia chombo hicho ambacho kwa miongo mingi kimekuwa muhimu kupitisha taarifa muhimu kwenda kwa jamii na pia kuwapa wanajamii fursa ya kueleza mawazo yao katika ujenzi wa maisha yao, Umoja wa Mataifa umeamua maadhimisho ya mwaka huu yalenge kuzienzi redio za kijamii ambazo zinatoa fursa kwa watu walioko mashinani.

Sauti
3'28"