Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

Picha: UNICEF/Al-Zikri

Vijana waonywa dhidi ya matapele wanaposaka ajira katia sekta ya mafuta, Uganda

Kutokana na kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana katika nchi nyingi duniani, baadhi ya vijana wamejikuta katika mazingira ya kunyang’anywa kidogo walichonacho kupitia mikono ya matapeli.

Hali si tofauti nchini Uganda mabapo uzalishaji wa mafuta unanyemelea katika Bonde la Ufa la Ziwa Albert.

Taarifa zinasema tayari vijana kadhaa wamekuwa waathirika wa utapeli kwa kulipa pesa kama moja ya masharti ya kupata kazi mbalimbali katika makampuni ya mafuta yaliyoanza upya kufanya kazi baada ya kusitishwa kutokana na mlipuko wa COVID-19.

Sauti
3'53"
UN Tanzania/Ahimidiwe Olotu

Kumhoji Rais alikuwa anatumwa mwandishi mwanaume badala ya mwanamke-Bi.Mongela

Bi Getrude Mongela kupitia katika mahojiano yaliyofanywa na Stella Vuzo wa Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIC Tanzania, mwanamke huyo aliyekuwa Katibu Mkuu wa mkutano wa 4 wa wanawake uliofanyika Beijing miaka 25 iliyopita, anaeleza mafanikio ambayo yamefikiwa katika kumpa nafasi mwanamke, akianza na mfano hali ilivyokuwa awali katika vyombo vya habari.

Sauti
3'31"
UN/Andrew Kahwa

Mazingira yamefanya familia yangu ipate lishe bora na kipato-Mfugaji wa Sungura Tanzania

Bi Joyce Ballo wa Ifakara Morogoro Tanzania, anasema uamuzi wa wakulima wa mbogamboga na miti katika eneo lake wa kutumia njia mbadala za kutunza mazingira kwa kuamua kutotumia dawa na mbolea zenye sumu, kumempa fursa ya kupata kipato na lishe kwa familia yake. 

 

Kupitia katika mahojiano haya yaiyofanywa na John Kabambala wa redio washirika KidsTime FM ya Morogoro, mkulima huyo anaeleza uhusiano wa utunzaji mazingira na chanzo chake cha sasa cha kipato, yaani ufugaji wa sungura ambapo anaweza kuingiza takribani dola 15 kwa wiki kutokana na shughuli hiyo. 

Sauti
3'36"
World Bank / Sarah Farhat

Mabaraza ya watoto Tanzania yalianzishwa ili kuwashirikisha watoto katika kupanga mstakabali wao

Ni wazi kwamba ili kujenga jamii iliyo bora, ni muhimu kuanzia chini katika mizizi ya jamii yaani kuwaelimisha watoto kuhusu wajibu na haki zao. Lakini ni wazi pia kuwa lengo hilo linaweza kufanikiwa kwa ufanisi zaidi ikiwa watoto wenyewe watashirikishwa kuanzia ngazi ya awali kwa wao wenyewe kutoa maoni yao na pia kupata fursa nyingine kama za kuwa na mahali pa kutoa taarifa iwapo haki zao za utoto na kijamii zinapokwa na hivyo kuathiri ustawi wao.

Sauti
4'2"
UN News/Assumpta Massoi

Licha ya changamoto, mwanamke wa kijiji bado anajitahidi kujikwamua

Hivi karibuni dunia imeadhimisha siku ya mwanamke wa kijijini ikimulika harakati zao na changamoto wanazokumbana nazo hasa wakati huu wa janga la ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19. Kundi hili limegubikwa na changamoto kama vile huduma za kijamii na kiuchumi na hivyo janga la COVID-19 kuwa sawa na kuongeza chumvi kwenye kidonda.

Sauti
3'54"
UN News/ John Kibego

Ugunduzi wa rasilimali ya mafuta huwa ni wa kujivunia lakini unakuja na changamoto zake

Ugunduzi wa rasilimali ya mafuta hua ni wa kujivunia kwani huleta fursa nyingi zikwemo ajira, ukwaji wa miji, viwanda na hata uchumi wa taifa kwa ujumla.

Lakini kwa upande mwingine hua na madhara kwa mazingira na jamii ambayo huathiri zaidi watu wa kipato cha chini katika jamii husika.

Uganda inajiandaa kuanza kuzalisha mafuta katika eneo la Bonde la Ufa la Ziwa Albert ambapo sasa wanamazingira wanaonya kuhusu athari za viwanda vya mafuta wakati ambapo misitu ya asili inazidi kuchafuliwa kwa ajili ya kilimo na makaazi.

Je, wanasema ini?

Sauti
3'50"
UN News/ John Kibego

Waganga wa asili wa mifupa wapongeza huduma ya picha za X-ray Uganda

Licha ya juhudi za kimataifa za kuimarisha huduma za afya kwa kuchagiza wagonjwa kusimamiwa na watalaam wa afya kwenye hospitali zinazotambulika, waganga wa asili wamesalia na ushawishi mkubwa katika utoaji wa tiba kwa jamii. Hii ni kutokana na imani ya baadhi ya wanajamii na pia uhaba wa fedha zinazotakiwa kwenye hospitali za kipekee na  mapungufu katika hospitali za serikali.

Sauti
4'7"
Arne Hoel/World Bank

Vijana Uganda wakaribisha sheria ya kugombea chini ya umri wa miaka 30.

Kwa miaka 25 ya katiba ya Jamhuri ya Uganda, vijana walio chini ya umri wa miaka 30 wamekuwa wakisaka fursa ya kukubaliwa kugombea nafasi mbalimbali za kisiasa katika serikali za mitaa kutokana na vizuizi vya sheria za uchaguzi.

Vijana hao wamekuwa wakiona kwamba hali hiyo inawanyima nafasi ya kushika nafasi za  kisiasa na hatimaye kupona ukosefu wa ajira. Hata hivyo mwezi huu wa Oktoba umekuja na marekebisho ambapo bunge limepitisha mswada wa kuondoa kikwazo hicho na kuruhusu vijana kuanzia umri wa miaka 18 kugombea nafasi mbalimbali za kisaiasa.

Sauti
3'46"