Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kupata utambuzi na tuzo maana yake kazi yako imeonekana na ni fursa kufanya zaidi

Kupata utambuzi na tuzo maana yake kazi yako imeonekana na ni fursa kufanya zaidi

Pakua

Shirika lisilo la kiserikali la CAMFED nchini Tanzania ni moja ya mashirika yanayopambana kuhakikisha yanachangia katika kutimiza angalau malengo machache kati ya malengo 17 ya maendeleo endelevu, SDGs. Shirika hili kwa kiasi kikubwa limejikita katika lengo namba 4 linalozungumzia elimu bora na lengo namba 5 linazungumzia usawa wa kijinsia, yote hayo yakiwa yanalenga kutomwacha nyuma mtu yeyote katika maendeleo ya ulimwengu ifikapo mwaka 2030. 

Kupitia makala hii, John Kabambala wa redio washirika Kids Time FM ya Morogoro Tanzania amehudhuria hafla ya kutambua mchango wa wasichana na wanawake waliopitia katika mikono na mafunzo ya shirika la CAMFED miaka mitano iliyopita kupitia mpango wa Dunia yangu bora na sasa wanawake hao wanawasaidia wasichana wengine walioko katika mazingira magumu.

Audio Credit
Grace Kaneiya/ John Kabambala
Audio Duration
4'1"
Photo Credit
UN News Kiswahili