Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UN News

Ninasisitiza sana vijana kuchukua fursa zilizopo sasa, bila kusubiri- Professa Nyoni

Ujumuishaji wa vijana katika ngazi za maamuzi na za kimaendeleo ni suala ambalo linasisitizwa kila uchao. Lakini maandalizi ya vijana hao katika nafasi mablimbali yanafanyika shuleni na pia kwenye vyuo vikuu. Mmoja wa watoa elimu ambao wanasaidia vijana sio tu kutambua uwepo wa fursa lakini pia kutumia fursa hizo ni Professa Nyoni ambaye kwa kutambua nafasi finyu zilizopo anahimiza vijana kuchukua fursa zilizopo sasa. 

Sauti
3'17"
World Bank/Arne Hoel

Vijana na mikakati ya kuepuka changamoto ya ukosefu wa ajira, Uganda

Katika zama hizo ambazo ulimwengu unakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa watu wengi, zipo sababu nyingi zinazochangia uwezekano wa kijana kupata fursa ya ufadhili wa elimu au kuajiriwa ili kuepuka changamoto za kutokuwa na ujuzi unaoendana na soko la ajira.  Sababu hizo ni pamoja na tabia au mienendo ya kijana husika katika jamii na malengo ya kijana binafsi. Nchini Uganda, ukosefu wa ujuzi unaoendana na kazi zilizopo ni miongoni mwa changamoto kubwa ambazo serikali na wadau wake wa mafuta wamekuwa wakishughulikia kwa karibu muongo mmoja uliopita.

Sauti
4'
UNnewskiswahili/Patrick Newman

Ibua Afrika ni daraja kati ya wanawake na wawekezaji nchini Kenya- Mumbi Ndung'u

Wakati dunia ikihaha kutumiza malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa, nchi na watu binafsi wanaibuka na njia bunifu kwa ajili ya kusongesha malengo hayo mbele kuelekea ukomo wake mwaka 2030. Moja wa watu ambao wamebuni njia mpya za kuwezesha makundi katika jamii ikiwemo wanawake na vijana na Mumbi Ndung'u mwanzilishi wa shirika la Ibua Afrika ambayo ilichipukia kwenye mitandao ya kijamii lakini sasa ikitumia jukwa mbali mbali kuwakutanisha wawekezaji na wadau wengine na vijana na wanawake kwa ajili ya kuendeleza jamii.

Sauti
3'45"
UN News/ John Kibego

Nyasi vamizi zageuka fursa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi nchini Uganda

Mabadiliko ya tabianchi yanazidi kusababisha wasiwasi miongoni mwa jamii za wafugaji Afrika na kwingineko ulimwenguni hasa kutokana ukame wa muda mrefu. Hata hivyo, nchini Uganda hatua zinachukuliwa ambapo wameanza kubaini nyasi zinazoweza kuhiili mabadiliko haya ya tabianchi na hatimaye kuzihamishia katika maeneo mbalimbali ya nchi ili ziwasaidie badala ya kutegemea malisho asilia katika eneo fulani.

Mmoja wa wale ambao wamevalia suala hilo njuga ni Mbunge wa Kaunti ya Butemba wilaya ya Kyankwanzi Innocent Pentagon Kamusiime ambaye amepanda nyasi aina ya  Kikuyu.

Sauti
3'42"
FAO/IFAD/WFP/Petterik Wiggers

Uganda yahaha kuinua uzalishaji wa bidhaa za mifugo

Katika juhudi za kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu au SDGs na kuinua uchumi wa taifa Uganda imeamua kuchukua hatua mathubuti katika sekta mbalimbali ikiwemo ya ufugaji. Hivi sasa kupitia ongezeko la uzalishaji wa bidhaa za mifugo kwa ajili ya mauzo nje ya nchi, Uganda imelivalia njuga suala la kuwekeza katika teknolojia za kisasa, wakati huu ambapo nchi za Ulaya na China zimefungua milango kwa kununua bidhaa za mifugo na kilimo kutoka Uganda.

Sauti
3'57"
WFP/Jean-Fidele Ebenezer

Wakimbizi waomba msaada kukuza kipaji cha usanii Uganda

Mizozo hufifisha ndoto za vijana wengi baada ya wao kulazimika kufungasha virago mara nyingi kwa ghafla kitu ambacho huvunja mawasilaino na hatimaye mahusiano kwani kila mmoja husaka hifadhi popote pale kuna usalama bila kujali marafiki na akraba zake.

Wengine hupoteza mali zao na kulazimika kuanza maisha mapya ya kutegemea wahisani.

Sauti
3'44"
MONUSCO/TANZBATT/Taji Msue

Mradi wa kuoka mikate unaofadhiliwa na UN umeokoa familia yangu:Bichuna

Mradi wa Umoja wa Mataifa wa kuwasaidia waathirika wa ukatili wa kijinsia na kingono (SEA) katika mizozo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, umeendelea kuleta nuru kwa wanawake wengi na familia zao DRC ambayo imeghubikwa na vita kwa miongo sasa. Maelfu ya wanawake wamepitia ukatili huo na wengine hata kukata tamaa hadi pale mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO na ofisi maalum ya miradi ya kuwasaidia waathirika wa SEA kuanza kufanya kazi.

Sauti
3'46"
UN News/Assumpta Massoi

Je wajua kuwa ukubwa wa ziwa Tanganyika unazidi kupungua?

Nchini Tanzania, Ziwa Tanganyika lililopo mkoani Kigoma lasifika kwa kuwa la pili kwa kuwa na kina kikubwa zaidi duniani. Hata hivyo, kina na ukubwa wa ziwa vinapungua kutokana na mabadiliko ya tabianchi na shughuli za binadamu. Miongoni mwa mashuhuda wa hali hiyo ni Bwana  Kassim Govola Mbingo ambaye ni mhifadhi mkuu katika makumbusho ya Dkt. David Livingstone mjini Ujiji mkoani Kigoma. Katika mahojiano yake na Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Kiswahili ya  Umoja wa Mataifa anafafanua

Sauti
3'55"
UNDP video

Juhudi za kukabilana na ukimwi katika maeneo ya mafuta,Uganda

Mwingiliano wa jamii kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo uhamiaji, mizozo na kusaka fursa za kiuchumi huchochea mambukizi ya ugonjwa wa ukimwi na Hepatitis B yani homa ya ini na magonjwa mengine ya zinaa kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya ulimwenguni WHO.

Tishio hili ni dhahiri nchini Uganda hususan katika maeneo ya mpakani yenye shughuli za uchimbaji wa mafuta ambapo kando na ukimwi kuna tishio la ebola kutokana na wimbi la wakimbizi wanaoingia kutoka  nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

Sauti
3'56"
UN-Habitat/Julius Mwelu

Kijana kutoka Nairobi Kenya aupa kisogo uhalifu na sasa anajihusisha na utunzaji wa mazingira

Kutana na Fredrick Okinda ni mmoja wa vijana waliokuwa wahalifu sugu katika mtaa wa mabanda wa Korogocho ulio mjini Nairobi, Kenya. Kama wahenga walivyonena kufanya kosa si kosa kosa kubwa ni kurudia kosa. Amejifunza kutokana na makossa na kuamua kubadili Maisha yake na ya vijana wenzie waliopitia njia kama yake. Kwa sasa Fredrick ni kiongozi wa kikundi kwa jina Kombgreen Solutions kinachowaleta pamoja vijana walio katika uhalifu, kuwasaidia kubadili tabia na kushiriki katika huduma za jamii hasa utunzi wa mazingira.

Sauti
3'43"