Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uganda yahaha kuinua uzalishaji wa bidhaa za mifugo

Uganda yahaha kuinua uzalishaji wa bidhaa za mifugo

Pakua

Katika juhudi za kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu au SDGs na kuinua uchumi wa taifa Uganda imeamua kuchukua hatua mathubuti katika sekta mbalimbali ikiwemo ya ufugaji. Hivi sasa kupitia ongezeko la uzalishaji wa bidhaa za mifugo kwa ajili ya mauzo nje ya nchi, Uganda imelivalia njuga suala la kuwekeza katika teknolojia za kisasa, wakati huu ambapo nchi za Ulaya na China zimefungua milango kwa kununua bidhaa za mifugo na kilimo kutoka Uganda.

Juhudi hizo za serikali ni pamoja na uzinduzi wa mradi kabambe ambao utahakikisha matumizi ya tekinolojia za kisasa katika kuuimarisha ubora na wingi wa bidhaa za mifugo.

Ili kupata ufafanuzi zaidi wa juhudi hizo John Kibego  amezungumza na Naibu Waziri wa Huduma za umma, David Karubanga baada ya uzinduzi wa mradi kabambe unaotanguliza kutoa mafunzo kwa jamii walengwa.

 

Audio Credit
Brenda Mbaitsa/ John Kibego
Audio Duration
3'57"
Photo Credit
FAO/IFAD/WFP/Petterik Wiggers