Juhudi za kukabilana na ukimwi katika maeneo ya mafuta,Uganda

9 Januari 2020

Mwingiliano wa jamii kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo uhamiaji, mizozo na kusaka fursa za kiuchumi huchochea mambukizi ya ugonjwa wa ukimwi na Hepatitis B yani homa ya ini na magonjwa mengine ya zinaa kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya ulimwenguni WHO.

Tishio hili ni dhahiri nchini Uganda hususan katika maeneo ya mpakani yenye shughuli za uchimbaji wa mafuta ambapo kando na ukimwi kuna tishio la ebola kutokana na wimbi la wakimbizi wanaoingia kutoka  nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

Hata hivyo kampuni ya mafuta ya CNOOC Uganda Limited imeamua kuchukuwa hatua kuhamasisha jamii kuhusu mambukizi ya ukimwi VVU katika eneo inalofanyia kazi zake, la Buhuka-Kyangwali. Je, kuna mafanikio yoyote au nini zaidi kinatakiwa? Basi ungana na John Kibego katika makala ifuatayo.

Audio Credit:
UN News/John Kibego
Audio Duration:
3'56"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud