Je wajua kuwa ukubwa wa ziwa Tanganyika unazidi kupungua?
Pakua
Nchini Tanzania, Ziwa Tanganyika lililopo mkoani Kigoma lasifika kwa kuwa la pili kwa kuwa na kina kikubwa zaidi duniani. Hata hivyo, kina na ukubwa wa ziwa vinapungua kutokana na mabadiliko ya tabianchi na shughuli za binadamu. Miongoni mwa mashuhuda wa hali hiyo ni Bwana Kassim Govola Mbingo ambaye ni mhifadhi mkuu katika makumbusho ya Dkt. David Livingstone mjini Ujiji mkoani Kigoma. Katika mahojiano yake na Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa anafafanua
Audio Credit
Grace Kaneiya/ Assumpta Massoi/ Kassim Govola Mbingo
Audio Duration
3'55"