Wakimbizi waomba msaada kukuza kipaji cha usanii Uganda

15 Januari 2020

Mizozo hufifisha ndoto za vijana wengi baada ya wao kulazimika kufungasha virago mara nyingi kwa ghafla kitu ambacho huvunja mawasilaino na hatimaye mahusiano kwani kila mmoja husaka hifadhi popote pale kuna usalama bila kujali marafiki na akraba zake.

Wengine hupoteza mali zao na kulazimika kuanza maisha mapya ya kutegemea wahisani.

Licha ya haya yote, vijana katika makaazi ya wakimbizi ya Kyangwali nchini Uganda hawajavunjika moyo kuhusiana na ndoto zao kuwa wanamuziki na wanatamthilia mahiri  huku wakipaza sauti za kuomba msaada wa vifaa wakiamini kwamba itakuwa chanzo muhimu cha mapato mbeleni.

Audio Credit:
UN News/John Kibego
Audio Duration:
3'44"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud