Vijana na mikakati ya kuepuka changamoto ya ukosefu wa ajira, Uganda

22 Januari 2020

Katika zama hizo ambazo ulimwengu unakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa watu wengi, zipo sababu nyingi zinazochangia uwezekano wa kijana kupata fursa ya ufadhili wa elimu au kuajiriwa ili kuepuka changamoto za kutokuwa na ujuzi unaoendana na soko la ajira.  Sababu hizo ni pamoja na tabia au mienendo ya kijana husika katika jamii na malengo ya kijana binafsi. Nchini Uganda, ukosefu wa ujuzi unaoendana na kazi zilizopo ni miongoni mwa changamoto kubwa ambazo serikali na wadau wake wa mafuta wamekuwa wakishughulikia kwa karibu muongo mmoja uliopita. Hata hivyo fursa ni finyu kutokana na ushindani mkali wa wale walio na uhitaji. Je, ni jinsi gani kijana anaweza kujihakikishia nafasi za ufadhili? Basi ungana na John Kibego aliyezungumza na kijana Simon Baluku ambaye mara kadhaa amefanikiwa kufadhiliwa na sasa ana vyeti vya kimataifa vya uchomeleaji wa vyuma na anazidi kupata matumaini katika maisha yake ya sasa na ya baadaye.

 

Audio Credit:
UN News/John Kibego
Audio Duration:
4'

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud