Kijana kutoka Nairobi Kenya aupa kisogo uhalifu na sasa anajihusisha na utunzaji wa mazingira

Kijana kutoka Nairobi Kenya aupa kisogo uhalifu na sasa anajihusisha na utunzaji wa mazingira

Pakua

Kutana na Fredrick Okinda ni mmoja wa vijana waliokuwa wahalifu sugu katika mtaa wa mabanda wa Korogocho ulio mjini Nairobi, Kenya. Kama wahenga walivyonena kufanya kosa si kosa kosa kubwa ni kurudia kosa. Amejifunza kutokana na makossa na kuamua kubadili Maisha yake na ya vijana wenzie waliopitia njia kama yake. Kwa sasa Fredrick ni kiongozi wa kikundi kwa jina Kombgreen Solutions kinachowaleta pamoja vijana walio katika uhalifu, kuwasaidia kubadili tabia na kushiriki katika huduma za jamii hasa utunzi wa mazingira. Fredrick alikutana na mwandishi wetu wa Nairobi Jason Nyakundi na kumueleza zaidi kuhusu kikundi chake na manufaa yake kwa vijana na jamii.

Audio Credit
UN News/Jason Nyakundi
Audio Duration
3'43"
Photo Credit
UN-Habitat/Julius Mwelu