Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa kuoka mikate unaofadhiliwa na UN umeokoa familia yangu:Bichuna

Mradi wa kuoka mikate unaofadhiliwa na UN umeokoa familia yangu:Bichuna

Pakua

Mradi wa Umoja wa Mataifa wa kuwasaidia waathirika wa ukatili wa kijinsia na kingono (SEA) katika mizozo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, umeendelea kuleta nuru kwa wanawake wengi na familia zao DRC ambayo imeghubikwa na vita kwa miongo sasa. Maelfu ya wanawake wamepitia ukatili huo na wengine hata kukata tamaa hadi pale mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO na ofisi maalum ya miradi ya kuwasaidia waathirika wa SEA kuanza kufanya kazi. Wanawake wengi wamejitokeza na kupewa mafunzo mbalimbali ya ujasiriliamali ambayo yamewawezesha kuishi na kuhudumia familia zao yakiwemo mafunzo ya ufundi cherehani, ukulima wa uyoga, utengenezaji sabuni, ufugaji, upishi na uokaji wa mikate. Katika makala hii Flora Nducha anammulika mmoja wa wanake hao mjasiriamali wa kuoka mikate.

Audio Credit
Brenda Mbaitsa/ Flora Nducha
Audio Duration
3'46"
Photo Credit
MONUSCO/TANZBATT/Taji Msue