Kauli ya wahenga kuhusu samaki ni dhahiri kwa Wanjuhi Njoroge
Wahenga walinena kuwa samaki mkunje angali mbichi kwani akikauka hakunjiki! Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa mwanaharakati wa mazingira nchini Kenya, Wanjuhi Njoroge ambaye hivi sasa suala la miti na mazingira ni jambo ambalo ni sawa na kusema linatiririka kwenye damu ya mwili wake.