Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

'Liz Mazingira' asongesha kasi ya Hayati Profesa Wangari ya upanzi wa miti nchini Kenya

'Liz Mazingira' asongesha kasi ya Hayati Profesa Wangari ya upanzi wa miti nchini Kenya

Pakua

Nchini Kenya, harakati za upanzi wa miti zilizochochewa na Hayati Profesa Wangari Maathai bado zinazidi kushika kasi kila uchao hasa wakati huu ambapo harakati hizo zinaongozwa na msichana Elizabeth Wanjiru Wathuti al maarufu Liz Mazingira mwenye umri wa miaka 23. Liz Mazingira ametambuliwa sana nchini Kenya na pia Kimataifa kwa juhudi zake za utunzaji wa mazingira kwa njia ya upanzi wa miti, na kwa kuhamasisha  wengine kufanya hivyo, baada ya kupanda mti wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka saba. Je sasa anafanya nini? Mwandishi wetu wa Nairobi Kenya, Jason Nyakundi amezungumza naye na kuandaa makala hii.

Audio Credit
Flora Nducha
Sauti
4'8"
Photo Credit
UNMISS/Eric Kanalstein