IFAD yarejesha matumaini ya wakulima wa milimani Morocco

28 Oktoba 2019

Nchini Morocco mradi unaofadhiliwa na mfuko wa maendeleo ya kilimo wa Umoja wa Mataifa, IFAD umeendelea kuwa na mafanikio makubwa hususan kwa wanufaika ambao ni wakazi wa milimani. Mradi huo ulioanza mwaka 2011 na unatamatishwa mwaka huu wa 2019  unalenga watu 33,000 wengi wao wakiwa ni wakulima na wafugaji wadogo ambao ni pamoja na wanawake, vijana na wakulima wasiomiliki ardhi. Makundi haya ni yale ambayo yanaathirika na mnyororo wa thamani wa mazao kama vile matufaha na mizeituni.

Na sasa mradi huu wa IFAD umefanikiwa lengo lake la kupunguza umaskini kwa njia ya  ukuaji endelevu wa vipato vya wanawake, wanaume na vijana maskini vijijini. Je ni nini kimefanyika? Ungana basin a Brenda Mbaitsa.

Audio Credit:
Arnold Kayanda/Brenda Mbaitsa
Audio Duration:
3'

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud