Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jinamizi la ndoa za mapema katika jamii ya wafugaji wa Kiturkana, Kenya

Jinamizi la ndoa za mapema katika jamii ya wafugaji wa Kiturkana, Kenya

Pakua

Ndoa za mapema ni jinamizi kubwa lilalowandama watoto wa kike hasa katika jamii za wafugaji duniani kote, kutokana na tabia ya kulinganisha mtoto wa kike na maelfu ya mifugo. Jamii hizo ni pamoja na Karamajong Kaskazini Mashairki mwa Uganda, Toposa wa Kusini mashariki mwa Sudani Kusini na Masai na Turkana nchini Keenya.

Katika jamii ya Turkana Kenya, ndoa hizo ni sehemu ya utamaduni wao na unaathiri vibaya ustawi wa watoto wa kike na uke wao mbeleni.

Ili kufahamu kwa undani kuhusu miendendo ya ndoa hizo, ungana na mwandishi wetu John Kibego katika sehemu ya kwanza ya makala hii ambapo anazungmuza na msichana Betty Sike, manusura wa ndoa izo wakiwa katika mji wa Lokichar, Turkana South.

Audio Credit
Brenda Mbaitsa/John Kibego
Audio Duration
3'43"
Photo Credit
Photo: IRIN/A. Morland