Tuligundua kwa kukuza uchumi wa mwanamke, tutakuza uchumi wa jamii nzima-Paul Siniga

22 Oktoba 2019

Asasi ya African Reflections Foundation inayojishughulisha na utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs nchini Tanzania, kwa miaka mingi imejikita katika kuleta usawa wa kijinsia nchini humo kwa njia ya kukuza ushiriki wa shughuli za uchumi kwa wanawake. Asasi hiyo inatekeleza mradi wa kuwasaidia wanawake katika shughuli za kilimo kuanzia hatua ya mwanzo hadi hatua ya masoko. Paul Siniga, Mtendaji Mkuu wa asasi hiyo akihojiwa na Idhaa ya Kiswahilli ya Umoja wa Mataifa anafafanua namna wanavyotekeleza miradi hiyo.

 

Audio Credit:
Brenda Mbaitsa/Arnold Kayanda/Paul Siniga
Audio Duration:
3'15"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud