Mwaka 2018 umekuwa moto na wa moto
Matukio ya majanga yaliyoongezeka hivi karibuni kama vile athari za mvua kubwa na pepo za Monsoon, na moto wa msituni ni ishara kwamba athari za mabadiliko ya tabianchi ni dhahiri, kwa mujibu wa shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani-WMO.
Katika taarifa yake ya hivi majuzi shirika hilo limethibisha kwamba kiwango cha joto duniani kinaendelea kupanda haraka zaidi na kusababisha athari nyingi ikiwemo misitu kukauka na kuwa hatarini ya kushika moto haraka. Kwa undani wa hali hiyo ungana na Siraj Kalyango katika makala hii.