Teknolojia ya mtandao yatoa ajira kwa vijana Afrika
Ukuaji wa teknolojia ya matandao leo hii unatoa fursa kubwa ya ajira kwa vijana endapo wataamua kujituma na kuzitumia fursa hiyo vilivyo.
Mfano mzuri ni nchini Ghana ambako vijana wanatumia teknolojia ya mtandao kwa kutengeneza mavazi ya asili maarufu kama Kente na kuyauza kupitia mtandao baada ya kupata mafunzo ya kibiashara kutoka kwenye taasisi ya maendeleo nchini humo inayotoa mafunzo ya kibiashara. Kwa undani wa makala hiyo unagana na mwandishi wetu Siraji Kalyango.