Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwinoghe yanoga hadi kutambuliwa na UN

Mwinoghe yanoga hadi kutambuliwa na UN

Pakua

Hebu fikiria ni furaha iliyoje pale utamaduni wako tena ngoma ya kijadi inapotambuliwa na Umoja wa Mataifa kuwa ni tamaduni isiyogusika na ni muhimu kiasi ya kwamba inabidi iwekwe kwenye orodha maalum. Basi furaha hiyo iliwafikia wananchi wa maeneo ya kaskazini mwa Malawi mwezi Novemba mwaka huu wakati kamati ya turathi za tamaduni zisizogusika ilipokutana huko Mauritius na kutambua ngoma moja ya kitamaduni kutoka Malawi kuwa ni miongoni mwa tamaduni hizo. Ngoma hii ilianzia katika wilaya ya Karonga na hatimaye kati ya mwaka 1953 na 1955 iliboreshwa kutoka kabila la Indingala na huchezwa mathalani wakati wa kumsimika chifu au mtu anapofanya jambo la kishujaa kama vile anapoua Simba.  Wachezaji wa ngoma hii ni wanaume na wanawake vijana na kwa undani zaidi hali inakuwa vipi,Ungana na Assumpta Massoi kwenye makala hii.

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
4'25"
Photo Credit
Maktaba