Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ufahamu wa Kiswahili wamwinua mwananchi wa Uganda miongoni mwa wakimbizi

Ufahamu wa Kiswahili wamwinua mwananchi wa Uganda miongoni mwa wakimbizi

Pakua

Lugha ya Kiswahili imeendelea kusambaa na kukita mizizi hata katika maeneo ambayo hapo awali haikuwa na nguvu. Na kuenea kwa lugha hiyo adhimu kunachagizwa na matukio tofauti tofauti iwe amani na hata wakati mwingine mizozo. Ni katika mazingira kama hayo ambapo mwananchi wa Uganda Nsungwa Anette Khadja ameitumia fursa ya uhitaji wa lugha ya Kiswahili katika kambi ya wakimbizi ya Kyangwali wilayani Hoima nchini humo kwa kujifunza Kiswahili na sasa anafundisha lugha hiyo kwa wanafunzi wakimbizi na wenyeji. Na vipi alianza safari yake hiyo, mwalimu Nsungwa anafafanua katika mahojiano yake na mwandishi wetu wa Uganda, John Kibego.

Audio Credit
Siraj Kalyango/John Kibego.
Audio Duration
3'44"
Photo Credit
UN News