Hatua zimepigwa lakini kuna fursa ya kulinda haki za watu wenye ulemavu Tanzania-Lihiru
Pakua
Takwimu za shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO zinakadiria kuwa takriban asilimia 80% ya watu wenye ulemavu wanaishi katika maisha ya ufukara .
Kwa mantiki hiyo unaendelea kuzichagiza nchi kote duniani kuhakikisha watu wenye ulemavu wanasaidiwa na kujumuishwa katika mipango yao ya maendeleo. Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazozingatia hilo kwa kupitia kupitia mikakati mbalimbali iliyoweka pamoja na utetezi wa haki za watu wanaoishi na ulemavu.
Ili kupata uelewa zaidi kuhusu suala hilo, Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa, UNIC Dar es Salaam, Tanzania amezungumza na Mhadhiri na mtetezi wa watu wenye ulemavu nchini humo , basi unagana nao katika Makala hii kupanda undani zaidi kuhusu masuala hayo
Audio Credit
Siraj Kalyango/ Stella Vuso
Audio Duration
3'25"