Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kundi la wasichana wakimbizi laleta burudani kwenye Umoja wa Mataifa

Kundi la wasichana wakimbizi laleta burudani kwenye Umoja wa Mataifa

Pakua

Mkataba wa kimataifa kuhusu wakimbizi umepitishwa rasmi wiki hii na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Licha ya kwamba mkataba huo hauna masharti ya kisheria lakini unatoa mapendekezo ya utaratibu wa kusaidia wakimbizi na nchi zinazowahifadhi pamoja na kuimarisha mazingira ya wakimbizi ili kubadili mtazamo wa kuona watu hao kama mzigo katika jamii na badala yake kukubalika kama sehemu ya jamii walikokimbilia. Katika kukaribisha hatua hiyo kumefanyika hafla maalum kwenye Umoja wa Mataifa ambapo kando na mijadala kulikuwa pia na burudani kupitia kundi la wasichana wakimbizi waliohamia Marekani kama taifa la tatu kufuatia mpango wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR. Ungana na Grace Kaneiya katika Makala ifuatayo.

Soundcloud
Audio Credit
Siraj Kalyango/ Grace Kaneiya
Audio Duration
3'47"
Photo Credit
UN News/Grece Kaneiya