Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sanaa ya uchongaji yahitaji uvumilivu:Kijana Augustino James

Sanaa ya uchongaji yahitaji uvumilivu:Kijana Augustino James

Pakua

Wahenga walinena"mstahimilivu hula mbivu" usemi unahitajika sana katika kazi ya sanaa hususan ya uchongaji ambayo wakati mwingine huchukua siku hata miezi kabla ya kuona mafanikio yake. Kutokana na changamoto za ajira kwa vijana kote duniani wengi wameamua kuendeleza vipaji vyao vya sanaa iwe ya kuimba, kuchora na hata kuchonga vinyago kama alivyo kijana  Augustino James mkazi wa Morogoro Tanzania. Augustino anasema  sanaa ya uchongaji ni nzuri, ina toa ajira na kukidhi mahitaji lakini ina changamoto kubwa inayostahili uvumilivu ambao vijana wengi si rahisi kuukumbatia. Kulikoni? Ungana na John Kabambala kutoka Radio washirika Tanzaniakids FM alitemtembelea msanii huyo wa uchongaji vinyago 

Audio Credit
Siraj Kalyango/John Kabambala
Audio Duration
3'16"
Photo Credit
Photo: Hans Andersen