Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Huduma za afya bado ni changamoto Burundi

Huduma za afya bado ni changamoto Burundi

Pakua

Afya nzuri na maisha bora, wakati mwingine hutegemea, huduma nzuri za matibabu. Umoja wa Mataifa umesisitizia hilo katika lengo namba 3 la malengo yake  ya maendeleo endelevu, SDGs au ajenda 2030 . Hata hivyo katika baadhi ya mataifa barani Afrika hasa yale masikini, huduma hizo huwa zina walakini. Mfano,nchini Burundi katika baadhi ya maeneo bado wakazi wamekuwa wanakumbwa na  usumbufu wa kupata huduma nzuri za afya. Hii inatokea licha ya taifa hilo kutoa huduma bure za afya kwa watoto na kinamama wajawazito, bado  imekuwa ni kero kubwa kupata huduma nzuri za afya. Serikali ya Burundi imechagiza hospitali za umma kuhakikisha zinatoa huduma nzuri kwa wagonjwa ikizingatiwa kuwa afya ni haki za msingi. Kutoka Bujumbura, Burundi ,mwandishi wetu wa Maziwa Makuu Ramadhani Kibuga amefuatilia suala hilo katika makala haya.

Audio Credit
Siraj Kalyango/Ramadhan Kibuga
Audio Duration
4'41"
Photo Credit
© UNICEF/UN0188875/Njiokiktjien