'Hatuhamihami" bali tunahama na tutarejea- Dkt. Laltaika
Mvutano mkubwa huibuka baina ya wakulima na jamii ya watu wa asili hususan ile ya wafugaji. Mvutano huo ni katika masuala ya matumizi ya ardhi ambapo mara nyingi wafugaji hulaumiwa kutumia ardhi kiholela kutokana na kuhama kwao wanaposaka malisho ya mifugo yao. Umoja wa Mataifa unasisitiza masuala ya matumizi bora ya ardhi kama njia ya kulinda tabianchi Je ni kweli wafugaji huhamahama? Na je kupitia wafugaji hasa wa jamii ya asili ,dunia inaweza kubadili mweleko wa sasa wa uharibifu wa mazingira na tabianchi. Assumpta Massoi amezungumza na Dkt.