Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

DR Congo yaorodhesha wakimbizi 6,000 toka Sudan Kusini:

Takribani wakimbizi 6000 wamewasili nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wakitokea majimbo ya Equatoria Sudan Kusini.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR watu hao ambao pia wanajumuisha raia wa Congo wanaongia kwenye eneo la Dungu na walianza kukimbia mwezi Desemba kama anavyothibitisha, Teresa Orango afisa habari wa Kanda ya Afrika ya Mashariki na Kati wa UNHCR alipozungumza na Flora Nducha..

(MAHOJIANO TERESA ORANGO)

Bora baridi kuliko mashambulizi huko Syria; wasema wakimbizi

Mzozo wa Syria ukiwa umeingia mwaka wa tano, wakimbizi waliosaka hifadhi kwenye bonde la Bekaa nchini Lebanon wanahaha kujinusuru na baridi kali. Theluji ya kwanza imeanguka na maelfu ya wakimbizi ambao tayari wamekumbwa na machungu, wanazidi kuhaha, na miongoni mwao ni Abu Hamada.

Yeye, mkewe na watoto wao 10 waliwasili Bekaa miaka miwili iliyopita na sasa wanahaka kuhakikisha kuwa wanapata joto la kutosha ili kunusuru familia yao. Vifaa vya kutoa joto, mafuta na makazi ni usaidizi wa Umoja wa Mataifa na wadau wake wa misaada lakini bado hali si shwari.