30 Oktoba 2020
Katika kuelekea siku ya miji duniani hapo kesho Oktoba 31, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Abtonio Guterres kupitia ujumbe maalum wa siku hiyo amesema miji imebeba gharama kubwa ya janga la corona au COVID-19 lakini jamii katika miji hiyo zimedhihirisha thamani yake katika kukabiliana nalo.
Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP kwa kushirikiana na serikali ya Kenya leo wamezindua mpango wa ugawaji fedha taslim kwa familia 24,000 mjini Mombasa katika makazi yasiyo rasmi ambao Maisha yao yamesambaratishwa na athari za janga la COVID-19.