30 DESEMBA 2020

30 DESEMBA 2020

Pakua

Katika Jarida la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea matukio ya mwaka 2020

-Mwaka 2020 ulitangazwa kuwa mwaka wa wauguzi na wakunga na shirika la afya duniani WHO

-Janga la corona au COVID-19  Machi mwaka huu lilitangazwa kuwa janga la kimataifa. Na kwa mujibu wa WHO nchi 222 duniani zimeathirika huku watu zaidi ya milioni 1 na laki 7 wakipoteza maisha na wengine zaidi ya milioni 79 wameambukizwa ugonjwa huo

-Huko Lebanon kulizuka mlipuko mkubwa uliosababishwa na mitungi ya gesi mjini Beirut na kusambaratisha maisha ya watu, kukatili ya wengine, kujeruhi na kuharibu miundombinu

-Vimbunga navyo vilishika kasi kubwa hususan Amerika ya Kati na Kusini hasa kimbunga Etta

-Nchini Msumbiji hasa kwenye jimbo la Cabo Delgado machafuko yalizuka mapema mwaka huu na kufurisha maelfu ya watu yakiambatana na ukatili wa hali ya juu ikiwemo watu kuuawa, kukatwa vichwa, kubakwa na kujetuhiwa

-Mpango wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika  wa kulinda amani Darfur Sudan, UNAMID unafunga pazia kesho Desemba 31 baada ya takriban miaka 13

-Na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia salam zake za mwaka mpya ameisihi dunia kuungana kumaliza janga la mabadiliko ya tabianchi, kutokomeza COVID-19 na kuufanya mwaka 2021 kuwa mwaka wa uponyaji na matumaini

Audio Credit
UN News/Flora Nducha
Sauti
11'45"