Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

28 DESEMBA 2020

28 DESEMBA 2020

Pakua

Karika jarida la mada kwa kina hii leo Flora Nducha anakuletea

- Mashirika ya Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na la mpango wa chakula WFP kwa kushirikiana na serikali ya Ethiopia wamewafikishia msaada wa chakula wakimbizi 25,000 kutoka Eritrea walio katika kambi za wakimbizi jimboni Tigray

-Mpango wa Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika wa kulinda amani Darfur Sudan UNAMID umetoa mafunzo ya huduma ya kwanza, ushonaji barakoa na kutengeneza sabuni kwa wanawake wafungwa 30 mjini El Fasher

-Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR mpango wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu ncnhini humo MINUSCA umesema wananchi wametekeleza wajibu wao kwa kupiga kura ya Rais na wabunge jana licha ya uvumi wa  kuwepo udanganyifu

-Mada yetu leo tunaangazia wakimbizi katika kambi ya Kyangwali nchini Uganda wakizungumzia mwaka 2020 ulivyokuwa kwao na changamoto zake na kile wanachokitarajia mwaka ujao wa 2021

-Na mashinani tuko Ethiopia utamsikia mkulima akielezea baa la nzinge lilivyowaathiri mwaka huu

Audio Credit
UN News/ Flora Nducha
Audio Duration
12'9"