Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

29 Mei 2020

Kwenye Jarida la Umoja wa Mataifa leo ni siku ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa duniani :

-kwenye mada yetu ya kina baadhi ya wanawake wakazi wa mji wa Beni, jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, wameomba walinda amani wanawake kutoka Tanzania waendelee kuwaunga mkono kiuchumi na kijamii.

-Mlinda amani mwanamke kutoka Tanzania ambaye anahudumu katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, MONUSCO amethibitisha umuhimu wa uwepo wa askari wa kike katika ulinzi wa amani

Sauti
9'56"

28 Mei 2020

-Leo katika Jarida la Umoja wa Mataifa :

-Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM  la sema tushikamane kuchangia na kuwanusuru Wasyria na  COVID-19

- Kuelekea siku ya walinda amani duniani kesho Mei 29, tunamulika askari wanawake wa Tanzania.

-  Kutana na sajenti Desta anayesifika kwa kutengeneza magari ya UNMISS, Sudan Kusini

- Na kwenye Mashinani leo  tutakwenda nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kusikia jinsi  mchungaji mwanaume  alivyotumikishwa kingono na wanamgambo wanawake.

Sauti
13'21"

27 MEI 2020

Kwenya Jarida la Umoja wa mataifa hii leo
-COVID-19 yawa upenyo wa kutangaza maziwa ya kopo badala ya maziwa ya mama
-Tutasikia kauli ya mwandishi wa habari wa kujitegemea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na jinsi COVID-19 imebadilisha maisha ya familia yake.
-Pamoja na kuleta adha COVID-19 pia imekuwa faraja kwa wengine: tutasikia kutoka kwa Fundi Beatrice kutoka Tanzania anyeshona barakoa.

Sauti
12'31"

26 MEI 2020

Katika Jarida maalum la Habari hii leo Flora Nducha anakuletea

-Walinda amani wawili wanawake mmoja kutoka Brazili na mwingine kutoka India wameshinda tuzo ya Umoja wa Mataifa ya mwanajeshi mchagizaji wa masuala ya kijinsia kwa mwaka 2019. Wanajeshi hao Meja Suman Gawani kutoka India na kamanda Carla Monteiro Araujo kutoka Brazili watakabidhiwa tuzo hiyo Ijumaa ya 29 Meisiku ya walinda amani duniani.

Sauti
9'57"

25 05 2020

Katika Jarida maalum la habari hii leo Flora Nducha anakuletea

Leo ikiwa ni siku ya Afrika Umoja wa Mataifa umelisihi bara hilo na nchi zinazofanya uchaguzi kudumisha demokrasia wakiendesha uchaguzi huo hata wakati huu wa janga la virusi vya corona au COVID-19

 

Utafiti mpya uliochapishwa katika jarida la kitabibu la Lancet, umebaini kusambaa kwa ugonjwa wa saratani ya koo na sababu kuu ikiwa ni uwepo wa mashine za uchunguzi zinazofanya uchunguzi kupita kiasi hususan katika nchi za kipato cha kati.

 

Sauti
9'57"

22 Mei 2020

Leo Ijumaa tuna mada kwa kina tunamulika ukatili unaofanyika majumbani kutokana na zuio la kutoka nje lililowekwa kwa sababu ya ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19. Tunakwenda wilaya ya Hoima nchini Uganda, wanawake wanalalama, wanaume halikadhalika, ndani hakukaliki, na msemo wa "nyumba ni sufuria" umeshamiri. Tutakuwa na muhtasari wa habari ukibisha hodi Kairobangi na Ruai nchini Kenya, tutaenda Bangladesh na leo neno la wiki tunamulika methali na mchambuzi wetu anatoka Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya. Karibu na mwenyeji wako ni Flora Nducha.

Sauti
11'22"

19 Mei 2020

Hii leo tunamulika COVID-19 na athari zake kwa watu wasio na chakula ambapo ripoti inasema umaskini utaua watu zaidi kuliko virusi vyenyewe. Kuelekea siku ya nyuki duniani kesho, tumezungumza na wanahabari wanaofuga nyuki Tanzania. Nchini Kenya madhehebu ya kikatoliki yaunga mkono upanzi wa miti, makala tunatamatishia huko Kakonko mkoani Kigoma na mashinani tunabisha hodi Kenya. Mwenyeji wako ni Flora Nducha.

Sauti
12'48"

18 Mei 2020

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema janga la virusi vya corona ni kengele ya kutuamsha sote hivyo ni wakati wa kushikamana na kusaka kinga na tiba. IAEA yapokea zaidi ya dola milioni 4 kusaidia nchi kupambana na COVID-19. UNHCR yagawa msaada kwa waomba hifadhi Libya kwa ajili ya COVID-19 na Ramadhan. 

Sauti
14'29"