Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

30 JUNI 2020

Leo ni siku ya mabunge duniani ambapo Umoja wa Mataifa unasema ni siku muhimu ya kutambua mchango muhimu wa mabunge katika kupaza sauti za wananchi na pia kushawishi uundaji wa sera. Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la idadi ya watu duniani UNFPA imesema ili kukabiliana na janga la kimyakimya la mila potofu hatua za haraka zinahitajika kukomesha ukeketaji (FGM), ndoa za utotoni na mila zingine ambazo zinathiri wanawake na wasichana. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbiz

Sauti
12'1"

29 JUNI 2020

Katika Jarida la habari za UN hii leo flora nducha anakuletea

-Umoja wa Mataifa nchini Somalia waipongeza setrikali kwa juhudi kubwa za upimaji na mapambano dhidi ya janga la corona au COVID-19

-Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalokabiliana na ukimwi UNAIDS Winnie Byanyima amesema huduma za afya kwa wote si biashara bali ni haki ya binadamu ya kila mtu

-Nchini Malawi kutana na baba ambaye ni mfano wa kuigwa na wanaume wengine katika malezi ya watoto kwenye jamii

Sauti
12'7"

25 JUNI 2020

Ikiwa leo ni siku ya mabaharia duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kuwa sasa ni wakati muafaka wa kuwapa mabaharia heshima wanayoistahili. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC imetangaza kutokomezwa kwa mlipuko wa 10 wa Ebola  mashariki mwa nchi hiyo ulioanza mwezi Agosti mwaka 2018. Nchini Sudan Kusini, ujumbe wa Umoja wa Mataifa UNMISS umewaondolewa wanafunzi wa eneo moja mjini Yambio jimboni Equitoria Magharibi adha ya kusomea chini ya mti kwa kuwajengea madarasa ambamo watasomea bila bughudha

Sauti
13'47"

24 JUNI 2020

Katika Jarida la Umoja wa Matafa hii leo Flora Nducha anakuletea

-Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameiasa dunia kufuata katiba ya Umoja wa Mataifa inayotimiza miaka 75 wiki hii katika kutatua changamoto za dunia ikiwemo janga la COVID-19

-Nchini Tanzania hospitali ya CCBRT ambayo ina asilimia 6 ya wahudumu wake wenye ulemavu imesema inachukua hatua zote kuwalinda dhidi ya COVID-19 na kutaka serikali kuweka miundombinu ya kuwasaidia watu wenye ulemavu wakati wa janga la COVID-19

Sauti
12'43"

23 JUNI 2020

Ikiwa leo ni siku ya wajane duniani Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametaka kuangaziwa zaidi kwa kundi linalosahaulika mara kwa mara, wajane, hususan wakati huu wa janga la ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19. Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa mpango wa Umoja huo nchini Somalia UNSOM, James Swan amesema ms

Sauti
14'9"

22 JUNI 2020

Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea

-UNADS yaonya kwamba hatua zisipochukuliwa sasa nchi za kipato cha chini na cha Wastani Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara zitaathirika zaidi na COVID-19 hasa kwa wagonjwa wa HIV wanaohitaji dawa za kupunguza makali ya ukimwi

-Nchini Kenya katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma kutana na muhubiri anayetumia kipawa chake kuelimisha wakimbizi na jamii inayowahifadhi kuhusu janga la COVID-19

Sauti
12'46"

19 JUNI 2020

Jaridani la Umoja wa Mataifa hii leo

-Kuelekea kesho siku yawakimbizi duniani,kwenye mada yetu kwa kina leo tutamulika namna uwepo wa ugonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19 unavyoathiri maadhimisho hayo duniani.

- Antonio Guterres kupitia ujumbe wake wa siku ya wakimbizi duniani ameeleza ahadi ya Umoja wa Mataifa kukomesha migogoro na mateso ambayo imesababisha watu takribani milioni 80 kuyakimbia makwao

Sauti
10'13"

18 Juni 2020

Jaridani la Umoja wa Mataifa hii leo
-  Ripoti mpya ya mwenendo wa kimataifa wa wakimbizi na watu waliotawanywa duniani ambayo imetolewa leo na UNHCR inasema asilimia moja ya watu wote duniani wamelazimika kufungasha virago na kukimbia makwao
- UNHCR yachukua hatua za ziada kudhibiti kusambaa kwa COVID-19 kambi ya wakimbizi Dadaab
-  MINUSCA na shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP wamepatia gereza la Ngaragba msaada wa vifaa vya kusaidia kuepusha kuenea kwa ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19
- Na kweny
Sauti
9'56"

17 JUNI 2020

Katika Jarida la Habaroi hii leo kutoka Umoja wa Mataifa Flora Nducha anakuletea

-  Bei ya chajo ya homa ya vichomi au  ‘Numonia’ imeshuka, na kuleta ahueni kwa nchi maskini umesema leo Umoja wa Mataifa

-Ikiwa leo ni siku ya kukabiliana na ongezeko la jangwa na ukame duniani Umoja wa Mataifa umeitaka dunia kuchukua hatua kulinda sayari tunayoishi kwani afya ya binadamu inategemea afya ya sayari hii

Sauti
9'58"

16 JUNI 2020

Wakati leo ikiadhimishwa siku ya kimataifa ya utumaji fedha kwa familia , Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa ombi kwa watu kila mahali kuwaunga mkono wahamiaji katika wakati huu ambapo fedha ambazo zinatumwa nyumbani kwa familia na wahamiaji hao zimepungua kwa zaidi ya dola bilioni 100. Machafuko mapya katika eneo la Kaskazini Magharibi mwa Nigeria yamewalazimisha watu 30,000 kufungasha virago na kukimbilia katika eneo la Maradi nchi jirani ya Niger. Pia utamsikia mshindi wa mchoro wa Emoji ya siku ya wakimbizi duniani mwaka 2020.

Sauti
12'57"