Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

18 Desemba 2020

18 Desemba 2020

Pakua

Ikiwa leo ni siku ya wahamiaji duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesema ni mwaka wa kutathmini jinsi janga la Corona au COVID-19 lilivyosababisha mamilioni ya watu kukumbwa na machungu ya kutengana na familia zao na kutokuwa na uhakika wa ajira, jambo ambalo limewapatia watu hisia halisi ambazo wahamiaji hukumbana nazo kila wakati kwenye maisha yao. 

Na kikosi cha 7 cha Tanzania, TANZBATT_7 kwenye kikosi cha kujibu mashambulizi, FIB cha  ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO kimetamatisha jukumu lake na kupatiwa nishani ya Umoja wa Mataifa.

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
11'28"