31 AGOSTI 2020
Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO, leo limechapisha utafiti wake wa kwanza wa athari za janga la corona au COVID-19 kwa mifumo ya afya duniani, hali ikoje? Waathirika wa mafuriko makubwa yanayokumba maeneo mbalimbali ya Mashariki mwa Afrika na kusababisha athari ikiwemo watu kupoteza kila kitu, hususan nchini Kenya wamelishukuru shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kuwasaidia.