Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

28 Februari 2020

Hakuna mgonjwa mpya wa Ebola huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC katika siku 7 zilizopita, ni moja  ya habari muhimu hii leo kwenye muhtsasari wa habari na kisha ni mada kwa kina leo tukijikita huko wilayani Bukoba mkoa wa Kagera nchini Tanzania, mwandishi wa Radio washirika ya Kasibante FM Nicolaus Ngaiza anazungumza na mkunga wa jadi. Neno la Wiki leo ni gidamu, wafahamu maana yake? Tumekwenda BAKIZA huko Zanzibar! Basi  ungana na  mwenyeji wako hii leo jaridani, Flora Nducha.

Sauti
9'41"

27 Februari 2020

Suala la matumizi ya bidhaa za uraibu kama vile pombe na madawa ya  kulevya miongoni mwa watoto ni kipaumbele cha ripoti mpya ya Bodi  ya udhibiti wa madawa ya kulevya duniani, ripoti ambayo imetolewa leo huko Vienna, Austria na ndio miongoni mwa taarifa zetu hii leo, bila kusahau apu mpya ya kusaidia mtu kutumia kwa faragha taarifa zake binafsi mtandaoni na pia tunabisha hodi Ujerumani kwa mkimbizi wa Syria ambaye baada ya kupitia machungu hii leo anapika vyakula na kuuzia watu kadhaa mashuhuri akiwemo Kansela wa Ujerumani Angela Merkel.

Sauti
9'56"

26 Februari 2020

Nchi kushindwa kuwasilisha taarifa zao kuhusu virusi vya Corona, ni changamoto kubwa katika kudhibiti kusambaa kwa virusi hivyo hatari, yasema WHO. Huko Nzara nchini Sudan  Kusini moto wa nyika waleta tafrani kubwa na nchini Mali, rubani wa ndege za kivita kutoka El Salvador asihi wanawake wajitokeza. Katika makala leo Saa Zumo kutoka radio washirika Pangani FM mkoani Tanga  nchini Tanzania azungumza na muuguzi mkunga mwanaume na mashinani tunarejea tena Syria, kunani? Basi ungana na Flora Nducha.

Sauti
12'12"

25 Februari 2020

Jaridani hii leo Flora Nducha anaanza na uzinduzi wa jopo la kusimamia masuala ya watu kufurushwa makwao, uzinduzi umefanyika Geneva, Uswisi kisha tunabisha hodi Chad ambako watu wamefurushwa na kukimbilia Darfur nchini Sudan. Nchini Myanmar mradi wa ILO waleta nuru kwa wafanyakazi wa viwanda vya kushona nguo na mabegi na makala ni mwendelezo wa masuala ya wakunga na wauguzi na mashinani tunamsikia mtoto mkimbizi wa ndani nchini Syria akisema kile afanyacho, kuuza maua ili kulisha familia yake. Karibu!

Sauti
11'47"

24 FEBRUARI 2020

Jaridani Flora Nducha leo Februari 24, 2020

-Guterres azindua wito wa kuchukua hatua ili kulinda haki za binadamu duniani

- Vitisho dhidi ya haki za binadamu vinaongezeka lakini pia suluhisho-Bachelet

-Wakimbizi wanaokimbia ukatili wapata kimbilio kupitia chifu mji wa Kaya, Burkina Faso

Kwenye makala tunaeleka nchini Uganda.

Sauti
12'1"

21 Februari 2020

Jaridani Februari 21, 2020 na Assumpta Massoi

Ikiwa leo ni Ijumaa pata Habari kwa Ufupi, mada kwa kina imejikita na wakunga ikiwa huu ni mwaka wa kuwaenzi wakunga na wauguzi.

Na katika neno la wiki inachambuliwa methali, Atekaye maji mtoni hatukani mamba.

Sauti
9'55"

20 Februari 2020

Jaridani Assumpta Massoi leo Februari 20, 2020

-Viongozi Sudan Kusini wanyima wananchi chakula kwa makusudi- Ripoti

- Mkutano wa mjadala kuhusu katiba unalenga kuhakikisha ujumuishwaji wa sauti za raia Somalia

-Hata baada ya kuvuka baharí ya Mediteranea bado maisha ni shubiri kwa wakimbizi-UNHCR

Kwenye makala tunaeleka Simiyu nchini Tanzania.

Sauti
12'

19 Februari 2020

Jaridani Februari 19, 2020 na Assumpta Massoi-

Pata habari ikiwemo:

- Tabianchi, matangazo ya biashara vyatishia mustakabali wa watoto duniani- Ripoti

-Dola milioni 59.4 zahitaji kunusuru watoto Niger 2020- UNICEF

-Doria za pamoja zaMINUSCA, CAR, zarejesha wakazi makwao

Makala tunaangazia upatikanaji wa huduma ya afya ya uzazi kambini.

Sauti
12'25"

18 Februari 2020

Sikiliza Jarida la Habari la Februari 18, 2020 na Assumpta Massoi

Pata Habari ikiwemo: Akiwa ziarani nchini Pakistan, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa apongeza Pakistan kwa juhudi zake kukabiliana na polio huku akisisitiza kuwa kutokomeza polio ni moja ya vipaumbele vya Umoja wa Mataifa.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR laelezea masikitiko yake kufuatia vifo wakati wakimbizi waking'ang'ania mgao wa chakula nchini Niger.

Na nchini Sudan Kusini idadi ya majimbo bado ni shubiri katika uundaji wa serikali ya mpito.

Sauti
11'20"

17 Februari 2020

Hii leo jaridani Assumpta Massoi anaanzia nchini Kenya ambako Umoja wa Mataifa umeanza kupatia mafunzo vijana 300 wa jeshi la huduma kwa vijana kwa lengo la kusaidia kudhibiti nzige wa jangwani waliovamia taifa hilo tangu mwezi Desemba mwaka jana. Kisha anakwenda Sudan Kusini ambako walinda amani wa Umoja wa Mataifa wamekarabati na kushehenisha vitabu kwenye maktaba ya watoto mjini Juba.

Sauti
12'20"