Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

29 DESEMBA 2020

29 DESEMBA 2020

Pakua

Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea

-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Kenya limetoa msaada wa Redio 10,000 zinazotumia nishati ya jua au sola ili kuwawezesha watoto wengi kutoka kaya masikini kusomea nyumbani wakisubiri kurejea shuleni

-Maefu ya watu waliokimbia mapigano Tigray Ethiopia wamepitia madhila mengi lakini kina mama wajawazito ni zaidi, leo utamsikia mmoja wa wakimbizi hao aliyelazimika kujifungulia ugenini.

-Nchini Tanzania shirika la chakula na kilimo FAO linawasaidia wakulima ili kupambana na tatizo la lishe duni na utapiamlo,utamsikia afisa lishe wa FAO Tanzania.

-Makala yetu leo inatupeleka Uganda kuangazia kazi za UNHCR kwa mwaka huu wa 2020 na changamoto zake katika kuwasaidia wakimbizi

-Na mashinani leo tutakuchezea wimbo wa kampeni ya kuhamasisha wanafunzi na wazazi kujiandaa kurejea shule salama na kuzingatia masharti dhidi ya corona.

Audio Credit
UN News/ Flora Nducha
Audio Duration
12'22"