Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

UN /Aliza Eliazarov

Balozi Mahiga wa Tanzania asema tamko la haki za binadamu lizingatie tamaduni na maadili ya taifa.

Wakati Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania ikiwa imepata uongozi mpya kufuatia uteuzi uliofanywa na Rais wa Taifa hilo la Afrika Mashariki, John Magufuli, Waziri wa Katiba na Mambo ya Sheria Dkt. Augustine Mahiga amezungumzia majukumu ya tume hiyo wakati  huu ambapo tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limetimiza miaka 71 tangu  kupitishwa.

Sauti
2'31"
WFP/Gemma Snowdon

Hatua mujarabu yachukuliwa kuhakikisha tabiri za hali ya hewa zina 'mashiko'

Mashirika 12 ya kimataifa yanayotoa msaada katika nchi zinazoendelea leo yamekuja pamoja kwenye mkutano wa 25 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP25 unaofanyika huko Madrid nchini Hispania  na kuzindua ushirika mpya kwa ajili ya kuboresha masuala ya utabiri wa hali ya hewa, maji na huduma za mabadiliko ya tabianchi  au Alliance for Hydromet Development.

Sauti
1'48"