Wahamiaji wana haki na wanasitahili usaidizi bila kujali wanakotoka-Nick Ogutu
Mkutano wa 16 wa kuhusu haki za binadamu, uhamiaji na vijana leo umeingia siku yake ya pili katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Mkutano huo wa kimataifa unaofanyika kila mwaka unawakutanisha wadau wa haki za binadamu kutoka kote duniani na mmoja wa waliohudhuria ni rais wa taasisi inayoitwa ‘Safari yangu’, inayosimamiwa na Chuo Kikuu cha Columbia cha hapa Marekani, Bwana Nick Ogutu.