Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

FAO/Giulio Napolitano

Kinyesi si taka tena Kakuma bali ni faida.

Wakimbizi Kakuma nchini Kenya wameshukuru na kupongeza mradi wa nishati mbadala unaoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Kenya, mfuko wa Bill Gates na shirika la Sanivation. 

Mradi huo unaotumia kinyesi cha binadamu kutengeneza nishati mbadala umebadilisha maisha ya wakimbizi hao.

Sauti
1'47"
Picha ya UN women

Hatua lazima zichukuliwe kukomesha mzunguko wa machafuko Mali:UN

Hatua za haraka lazima zichukuliwe na jumuiya ya kimataifa kukomesha mzunguko wa machafuko ya kijamii na umwagaji damu unaoendelea nchini Mali machafuko ambayo hadi sasa yameshakatili maisha ya watu 160.

Wito huo umetolewa leo na mtaalam huru wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa akiongeza kuwa mfululizo wa mashambulizi kwenye jimbo la Kati la Mopti yaliyofanyika Machi 23 yamefuatiwa na ghasia mpya Machi 26.

Sauti
3'35"
UNnewskiswahili/Patrick Newman

Bado wanawake hawawakilishwi kwa kiasi kikubwa Kenya , wanaopata nafasi wanathaminiwa:Laboso

Wanawake duniani koete ikiwemo nchini Kenya bado hawapewi nafasi kubwa ya kuwakilishwa katika masuala ya siasa na uongozi lakini kwa wachache wanaopata fursa hiyo wanafanya kazi nzuri na mchango wao kuthaminiwa amesema Joyce Laboso gavana wa kaunti ya Bomet nchini Kenya akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa.

Sauti
1'53"