Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

UNDP video

Kulikoni Doreen Moraa Moracha anasema yeye ni simulizi ya kupendeza?

Kuelekea siku ya UKIMWI duniani tarehe Mosi mwezi ujao wa Desemba, Doreen Moraa Moracha, msichana kutoka Kenya ambaye anaishi na virusi vya UKIMWI amekuwa changamoto kubwa katika kumaliza unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi au VVU. Doreen amekuwa akifanya hivyo kupitia mitandao ya kijamii na kubwa zaidi katika mahojiano  yake na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, UN NEWS Kiswahili  anajiita yeye ni simulizi ya kupendeza, kulikoni?

Sauti
5'43"
Picha ya UN/Marie Frechon (Maktaba)

Wanavyosema wakazi wa kambi ya wakimbizi ya Kyagwali nchini Uganda wkuhusu siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake?

Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na wasichana zinaendelea kuadhimishwa kote duniani.  Ukatili ambao Umoja wa Mataifa unasema sio tu unaathiri mamilioni ya kundi hilo na kukiuka haki zao za binadamu bali pia unaacha jeraha lisilokwisha katika akili na maisha ya wanawake na wasichana duniani. Sasa Umoja huo unahimiza nchi zote, mashirika, asasi za kiraia na wadau kuhakikisha wanapambana kwa kila njia kutokomeza jinamizi hili kwani ni chini ya asilimia 10 ya wanawake na wasicha wanaoathirika ndio wanaouripoti.

Sauti
3'29"
Photo: Sean Kimmons/IRIN

Jamii yashika usukani katika vita dhidi ya VVU CAR

Katika mapambano dhidi ya Virusi Vya UKIMWI, VVU na UKIMWI nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, vikundi vya kijamii vinavyoundwa na watu wanaoishi na VVU vinasaidia kusambaza dawa katika maeneo ambayo yana ugumu wa kufikiwa kutokana na usalama mdogo na uhaba wa huduma za kiafya, juhudi ambazo zimewasaidia wengi kama ilivyo katika vijiji vya Zemio. 

Sauti
3'32"
UNMISS\Nektarios Markogiannis

Tumechoka kubakwa hebu tuokoeni- Wanawake Sudan Kusini!

Siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake zikiendelea kuangaziwa duniani, nchini Sudan Kusini nako Umoja wa Mataifa umetumia kipindi hiki kutoa fursa kwa wanawake kupaza sauti zao huku ukimulika pia hatua za kuwawezesha kiuchumi wanawake hao.  John Kibego na taarifa kamili.

Mjini Juba, nchini  Sudan Kusini, maandamano yakiongozwa na Mwakilishi wa kudumu wa Umoja wa Mataifa nchini David Shearer akiambatana na wanawake na wanaume, kuashiria kampeni ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake wakipaza sauti sasa imetosha.

Sauti
1'59"
Photo: FAO/Carl de Souza

Mradi wa UN Women wa M4C waleta neema kwa wanawake Pasifiki

Katika visiwa vya Pacifiki kati ya asilimia 75 hadi 90 ya wachuuzi sokoni ni wanawake na kwa kutambua umuhimu wao na mchango wao katika jamii  shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN Women liliamua kuanzisha mradi wa masoko kwa kwa ajili ya mabadiliko au M4C kwa ajili ya kuwawezesha wanawake hao na familia zao. 

Sauti
2'27"