Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Dr wa hospitali inayoungwa mkono na UM DR Congo apata tuzo

Dr Denis Mukwege, mkuu wa hospitali ya Panzi mjini Bukavu iliyoko Kivu ya Kusini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ametunukiwa tuzo ya kiamataifa na ufalme wa Ubelgiji mwezi Mai mwaka huu kwa mchango wake katika jamii.

Tuzo hiyo ya kimataifa ambayo hutolewa kila baada ya miaka miwili humuendea mtu ambaye amechangia kwa kila hali kuendeleza maendeleo duniani.

MKURABITA yaitwalia Tanzania tuzo ya UM ya utumishi wa umma

Mpango wa kurasimisha rasilimali na biashara za wanyonge Tanzania MKURABITA umeisaidia Tanzania kujinyakulia tuzo ya utumishi wa umma Tuzo hiyo ambayo hutolewa kila mwaka na Umoja wa Mataifa hasa kwa kuangalia ubunifu wa kuweza kuharakisha huduma nzuri kwa umma.

Baada ya kushika nafasi ya pili mwaka jana mwaka huu Tanzania imeshika nafasi ya kwanza barani Afrika. Tuzo hiyo imetolewa sambamba na kongamano la kimataifa la utumishi wa umma linalofanyika jijini Dar es salaam Tanzania kuanzia Juni 20 na litakamilika june 23.

Waliowauwa walinda amani wa MONUSCO wahukumuwa DR Congo

Watu  wanne miongoni mwa tisa wanaodaiwa kuwa waasi waliowawa askari watatu walinda amani wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUSCO miezi tisa iliyopita wamekatiwa hukumu na mahakama ya kijeshi nchini humo.

Watu hao wamesomewa hukumu yao mjini Goma Kivu ya Kaskazini Mashariki mwa Congo, wilaya ambayo walitekeleza mauaji hayo baada ya kuvamia ofisi za Umoja wa Mataifa.  Na hukumu hizo ni kuanzia kifungo cha kifo, kwenda jela maisha na wengine miaka kadhaa.

Katika vita vya ukimwi Tanzania kuongeza elimu, madawa na utafiti:Dr Bilal

Serikali ya Tanzania inasema pamoja na kupiga hatua katika vita dhidi ya ukiwmi bado ina safari ndefu ingawa zaidi ya asilimia 50 ya waathirika wanapata dawa za kurefusha maisha.

Kwa mujibu wa Makamu wa Rais wa nchi hiyo Dr Mohammed Gharib Bilal aliyezungumza kwa kina na mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa mataifa Flora Nducha nia yao ni kufikia maambukizi sufuri, vifo sufuri na unyanyapaa sufuri dhidi ya ukimwi.

Ingawa bado ina changamoto Kenya inasema imepiga hatua katika vita vya ukimwi

Pamoja na kwamba mkutano wa ngazi ya kimataifa wa ukimwi ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa umekamilika lakini vita dhidi ya ukimwi vinaendelea.

Viongozina wawakilishi 3000 kutoka nchi zaidi ya 30 waliokuwa wakikutana wametoka na azimio la kuweka malengo ikiwa ni pamoja na kupunguza kwa asilimia 50 HIV ifikapo 2015, pia wanadhamiria kupunguza kwa nusu maambukizi ya HIV kwa wanaotumia mihadarati na kuhakikisha kwamba ahakuna mtoto atakayezaliwa na virusi vya HIV.

UM umezindua mpango kukabiliana na unyanyapaa kwa wenye HIV

Umoja wa Mataifa leo Juni 8 umezindua mpango maalumu wa kukabiliana na unyanyapaa kwa wafanyakazi wanaoishi na virusi vya HIV katika mada ya “unyanyapaa unachagiza maambukizi zaidi”.

Kampeni hiyo pamoja na kuzinduliwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York ambako wakuu wan chi na wawalikishi kutaoka mataifa zaidi ya 30 wanakutana kwa siku tatu kujadili hatua zilizopigwa na zipi mpya zichukuliwe katika vita vya ukimwi pia imezinduliwa katika ofisi mbalimbali za Umoja wa Mataifa kote duniani.

Gharama za matibabu katika nchi zinazoendelea ni changamoto:UM

Gharama ya matibabu hasa katika mataifa yanayostawi imetajwa kama changamoto kubwa katika vita dhidi ya magonjwa.

Kukabiliana na magongwa ni miongoni mwa malengo ya maendeleo ya milenia yaliyoainishwa na Umoja wa Mataifa baada ya wakuu wa nchi kuyapitisha mwaka 200, lakini imebainika kuwa watu wanaoishi katika umaskini wanaendelea kulemewa na mzigo wa kugharamia matibabu.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa bima ya matibabu  ni muhimu lakini sio mataifa yoye yanayomudu kuhakikisha hilo kwa watu wake.

Shirika la kimataifa la uhamiaji linasaidia watu wanaokimbia machafuko Abyei

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan umesema wakati maelfu ya watu wakikimbia jimbo la Abyei Sudan kutokana na machafuko na kuelekea Sudan Kusini, mashirika ya misaada yanaongeza juhudi za msaada wa kibinadamu.

Jumbe Omari Jumbe , msemaji wa Shirika la kimataifa la uhamiaji (IOM) amezungumza na Redio ya Umoja wa Mataifa hii leo juu ya hali katika eneo la Abyei na juhudi za IOM kuwasaidia wale wanaokimbia  machafuko jimbo hilo la Sudan.

Serikalia ya mpito ya Somalia lazima iafikiane:UM

Serikali ya mpito ya Somalia imeambiwa sasa umefika wakati wa kumaliza tofauti zao, na kuzingatia maslahi ya taifa.

Wito huo umetolewa na ujumbe wa braza la usalama la Umoja wa mataifa uliohitimisha mkutano wa kujadili hali ya Somalia mjini Nairobi Kenya.

Ujumbe huo umetoa muda wa wiki kadhaa hadi katikati ya Juni kwa Somalia kufikiri, kujadili na kuamua hatma ya taifa lao kwa kuitisha uchaguzi na kumaliza kipindi cha mpito kama ilivyopangwa.

IOM kusafirisha mamia ya wahamiaji waliokwama jangwani Chad

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kuanzia mwishoni mwa wiki hii wataanza kuwasafirisha maelfu ya wahamiaji waliokwama jangwani mpakani mwa Chad na Niger.

Wahamiaji hao ni wale wanaokimbia machafuko Libya, na kujikuta wamekwama kwa kukosa urafiri wa kuwafikisha Chad. Kwa mujibu wa IOM wahamiaji hao wengi kutoka Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara watasafirishwa kwa njia ya malori na watakuwa na safari ngumu na ndefu ya zaidi ya siku 20 jangwani.