Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikalia ya mpito ya Somalia lazima iafikiane:UM

Serikalia ya mpito ya Somalia lazima iafikiane:UM

Pakua

Serikali ya mpito ya Somalia imeambiwa sasa umefika wakati wa kumaliza tofauti zao, na kuzingatia maslahi ya taifa.

Wito huo umetolewa na ujumbe wa braza la usalama la Umoja wa mataifa uliohitimisha mkutano wa kujadili hali ya Somalia mjini Nairobi Kenya.

Ujumbe huo umetoa muda wa wiki kadhaa hadi katikati ya Juni kwa Somalia kufikiri, kujadili na kuamua hatma ya taifa lao kwa kuitisha uchaguzi na kumaliza kipindi cha mpito kama ilivyopangwa.

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa Somalia Balozi Augustini Mahiga anafafanua kuhusu uamuzi huo baada ya mkutano alipozungumza na Flora Nducha

(MAHOJIANO NA BALOZI MAHIGA)