Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Heri ya mwaka mpya 2018

Taswira ya jengo la makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani likiwa sambamba na majengo mengine. (Picha:UN/Maktaba)

Heri ya mwaka mpya 2018

Heri ya Mwaka mpya! Natumai u buheri wa afya ukiwa umepanga mikakati ya kusongesha mwaka huu! Kama kawaida ni miezi 12 lakini kila siku na jambo lake! Na Katika jarida letu hili maalum basi tunaangazia mwaka huu wa 2018!

Msikilizaji wetu huko mashinani amepanga kufanya nini? Na zaidi ya yote wana ujumbe upi kwa Umoja wa Mataifa?  Basi tuanzie nchini Uganda kwake mwandishi wetu John Kibego kisha tutaenda Tanga nchini Tanzania katika wilaya ya Pangani ambako Rajabu Mustafa wa Radio washirika Pangani FM amezungumza na wakazi wa eneo hilo.

Na vipi huko Burundi ? Mwandishi wetu wa Maziwa Makuu Ramadhani Kibuga amevinjari mjini Bujumbura na wananchi walifunguka. Mwenyeji wako ni Leah Mushi.