Burundi

‘Sijakomaa kuwa mwanamke’ asema mtoto nchini Burundi manusura wa usafirishaji haramu binadamu 

Kuelekea siku ya kimataifa ya usafiridhaji haramu binadamu, tunakwenda nchini Burundi ambako mtoto mmoja wa kike anasimulia jinsi wakati ana umri wa miaka 12 aliuzwa kwa gharama ya bia na ili kutumikishwa kingono katika nchi Jirani ya Tanzania.

Ziwa Tanganyika laendelea kufurika, Burundi wahaha, IOM na wadau waingilia kati

'Tutafanya nini iwapo maji yataendelea kujaa?’ Hilo ni swali lililogubika kila mtu: Wamiliki wa nyumba, wakandarasi wa ujenzi, wajenzi, wakulima, wachuuzi sokoni, wanafunzi, wasafiri na bila shaka wafanyakazi wa maendeleo na kibinadamu.
 

Wakimbizi wajumuishwa vyema kule walikokimbilia

Siku ya kimataifa ya wakimbizi duniani imeadhimishwa duniani kote tarehe 20 mwezi huu wa Juni. Maadhimisho haya yanafanyika wakati hivi sasa kuna zaidi ya watu milioni 80 duniani kote ambao wamelazimika kukimbia makazi yao kutokana na vita, ghasia na mateso na hivyo kujikuta wameacha kila kitu. 

Pamoja na kuifunga ofisi ya Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu, UN yaahidi kuendelea kuisaidia Burundi

Baada ya miaka minne ya shughuli nchini Burundi, Ofisi ya Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi, OSESG-B imefungwa rasmi jana Mei, 30, 2021.  Harumukiza Edmond wa televisheni washirika, Mashariki TV ana maelezo zaidi.

Sauti -
2'37"

Ofisi ya Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa UN nchini Burundi yafungwa rasmi 

Baada ya miaka minne ya shughuli nchini Burundi, Ofisi ya Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi, OSESG-B imefungwa rasmi jana Mei, 30, 2021.  

01 JUNI 2021

Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Leah Mushi anakuletea

-Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Burundi leo imefunga mlango rasmi baada ya hali ya amani na utulivu kurejea nchini humo utasiki taarifa  kutoka kwa washirika wetu Mashariki TV

Sauti -
13'39"

Japo tupo kambini lakini mkopo wa UNICEF umetukomboa kiuchumi

Kutokana na mabadiliko ya mifumo ya mvua, hali ambayo imekuwa ikileta maafa nchini Burundi na kusababisha mafuriko, maporomoko ya ardhi na kuharibu mazao, Jeannette Niyibigira, pamoja na mumewe na watoto 5, walilazimika kuyahama makazi yao ya Gatumba, na sasa wanaishi katika kambi ya Kiragaramang

Sauti -

26 Mei 2021

Hii leo jaridani Leah Mushi anaanzia na habari kuhusu haki za binadamu hususan wahamiaji wanaokufa maji huko bahari ya Mediteranea. Kisha Sudan Kusini ambako mradi wa UNIDO umeleta nuru na anakwenda Burundi ambako Ziwa Tanganyika maji yamefurika na kufurusha watu.

Sauti -
11'11"

Kama si UNICEF na mdau wake Foi En Action, nisingefika popote - Jeannette Niyibigira 

Kutokana na mabadiliko ya mifumo ya mvua, hali ambayo imekuwa ikileta maafa nchini Burundi na kusababisha mafuriko, maporomoko ya ardhi na kuharibu mazao, Jeannette Niyibigira, pamoja na mumewe na watoto 5, walilazimika kuyahama makazi yao ya Gatumba, na sasa wanaishi katika kambi ya Kiragaramango ambako kama si mkopo mdogo kutoka shirika la Foi En Action (Faith in Action) ambalo ni wadau wa UNICEF, Camp, maisha yangekuwa magumu zaidi.