Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Choo chako ni salama?

Choo huko African Quarters Hoima nchini Uganda. Picha: UM/John Kibego

Choo chako ni salama?

Utafiti umebaini kwamba ukosefu wa vyoo safi  na salama ni hatarishi kwa afya ya binadamu. Takwimu za mashirika ya ufya ulimwenguni kama WHO na wengine zinaonyesha kuwa jamii zinazoishi katika mazingira yasiyo na vyoo salama zipo katika athari za kupatwa na milipuko ya magonjwa yatokanayo ya ukosefu wa matumizi salama ya vyoo kama kipindupindu na magonjwa mengine.

Nchini Uganda katika  wilaya ya Buliso  baadhi ya wakazi wa vijijini hawana huduma safi na salama ya  vyoo, kitu ambacho ni hatarishi kwa afya ya wanavijiji hao. Mwandishi wetu John kibego alipata fursa ya kuzungumza nao ili kufahamu kulikoni?Tuungane naye basi kwa undani kwenye makala hii….