Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msanii mzaliwa wa Zanzibar ashinda tuzo ya Sanaa ya Turner:IOM

Bi Lubaina Himidi mzaliwa wa Zanzibar nchini Tanzania, mshindi wa tuzo ya Sanaa ya Turner. Picha: IOM_Darren O'Brien/Guzelian

Msanii mzaliwa wa Zanzibar ashinda tuzo ya Sanaa ya Turner:IOM

Msanii wa Uingereza Lubaina Himidi ametambulika kimataifa juma hili baada ya kazi yake ya saana inayotanabaisha siasa za kibaguzi na mchango wake katika masuala ya kumbukumbu ya utumwa  na uhamiaji kushinda tuzo ya mwaka huu ya Turner ambayo ni tuzo ya kimataifa ya sana aza kuchora.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM Bi Lubaina Himidi mzaliwa wa Zanzibar nchini Tanzania , kazi yake ya sanaa imetambulika kimataifa kufuatia habari za karibuni za wahamiaji kutoka barani Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara kuuzwa mnadani Libya kama watumwa.

IOM inasema hadi kufikia Desemba Mosi mwaka huu imeorodhesha zaidi ya wahamiaji 400,000 nchini Libya , lakini idadi kamili ya wahamiaji nchini humo inakadiriwa kuwa kati ya laki 7 na milioni moja.

Akiwa na umri wa miaka 63 , Lubaina Himidi sio tu kwamba ni mtu mwenye umri mkubwa zaidi kuwahi kushinda tuzo hiyo baada ya vikwazo vya umri kwa washiriki kuondolewa mapema mwaka huu , bali pia ni mwanamke wa kwanza mweusi kuwahi kushinda tuzo hiyo.

Bi Himidi ni miongoni mwa wasanii waanzilishi wa kuchagiza Sanaa ya Waingereza weusi na kazi yake siku zote inaonyesha masuala yanayowakabili watu wa afrika na historia ya ukoloni ikiwemo mambo ya utumwa.