Skip to main content

Chuja:

maji safi na salama

17 APRILI 2023

Hii leo jaridani tunasalia hapa makao makuu kukuletea yaliyojiri kwenye Jukwaa la kudumu la watu wa asili, na pia kukupeleka nchini DRC kumulika faida ya mradi unaofadhiliwa na Benki ya Dunia wa kupanda miti aina ya migunga. Makala tunaangazia SDG 17 na Mashinani tunakupeleka nchini Tanzania, kulikoni?

Sauti
12'55"
Kikosi cha Walinda Amani wa Tanzania, TANBAT 6 wanaohudumu chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati – MINUSCA wakitoa huduma ya maji safi na salama kwa jamii mjini Berberati mkoa wa Mambéré-Kadéï.
TANBAT6/Kapteni Mwijage

TANZBAT6 watoa huduma ya maji kwa wananchi nchini CAR

Kikosi cha sita cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wanaohudumu chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati – MINUSCA wametoa huduma ya maji safi na salama kwa vijiji vinavyokabiliwa na uhaba wa maji mjini Berberati mkoa wa Mambéré-Kadéï. 

Sauti
2'27"

23 MACHI 2023

Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina ambapo Mkutano wa 67 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW67 umekunja jamvi baada ya kufanyika kwa takribani wiki mbili! Maudhui yalikuwa ni vipi teknolojia na uvumbuzi vinaweza kumkwamua mwanamke na msichana katika zama za kidijitalitunaangazia, na Getrude Dyabene, Afisa kutoka Kituo cha Msaada wa Sheria na haki za binadamu nchini Tanzania atakueleza washiriki waliondoka na ujmbe gani.  Pia tunakuletea habari kwa ufupi za afya, maji safi na salama na biashara.

Sauti
12'33"
Mtoto akiwa amesimama karibu na pampu ya maji iliyozingirwa na maji ya mafuriko huko Gatumba nchini Burundi.
© UNICEF/Karel Prinsloo

UNICEF imetuepusha na maji yenye wadudu- Wakazi wa Cibitoke

Tukiwa tunaelekea ukingoni mwa wiki ya maji duniani , nchini Burundi mradi uliotekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kwa msaada wa serikali ya Japan umesaidia wakazi wa eneo la Cibitoke nchini Cibitoke siyo tu kuondokana na unywaji wa maji machafu  yenye wadudu, bali pia kuepusha watoto dhidi ya magonjwa na watoto wa shule kuondokana na zahma ya kutembea muda mrefu kwenda kuteka maji badala ya kwenda shuleni.

Jarida 14 Septemba 2021

Hii leo katika jarida tutasikia kuhusu mkutano wa 75 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA75 unaofungwa rasmi hii leo na kufunguliwa kwa mkutano wa 76 au UNGA76. Rais wake mteule Abdulla Shahid kutoka Maldives amehojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa na kusema tumaini ndio limesalia kuwa tegemeo kwa mabilioni ya watu duniani wakati huu wakihaha katikati ya janga la COVID-19, uharibifu wa mazingira, vita na majanga mengineyo. 

kwa habari hiyo na nyingine nyingi ikiwemo sauti kutoka mashinani na makala ungana na Assumpta Massoi 

Sauti
15'6"