Kujisaidia kwenye vifuko vya nailoni kumebakia historia- Mkazi wa Accra
Nchini Ghana, huko Afrika Magharibi ukosefu wa choo umekuwa ni adha kubwa kwa wakazi wa kitongoji kimoja maarufu kwa utalii kwenye mji mkuu Accra. Vifuko vya nailoni vilivyosheheni haja kubwa vilikuwa ni jambo la kawaida hadi Benki ya Dunia ilipoingilia kati na kusaidia mamlaka ya majisafi na majitaka ya jiij la Accra, GAMA. Sasa kuna ahueni na wananchi wamefunguka macho.