Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yatoa tani 70 ya vifaa vya Hispitali Yemen

Picha: WHO
Wahudumu wa WHO wafikisha tani 70 ya vifaa vya Hospitali Yemen. Picha: WHO

WHO yatoa tani 70 ya vifaa vya Hispitali Yemen

Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO, limepeleka  tani 70 za misaada ya kibinadamu ikiwemo vifa upasuaji kwajili ya hospitali katika mji mkuu Sana huko Yemen.

Msaada huu ambao ni mkubwa zaidi kupelekwa  chini Yemen tangu mwaka huu uanze, utasaidia mahitaji ya  wagonjwa wapatao 2000 ambao ni wagonjwa wa akili na upasuaji, na pia magonjwa yanaohitaji uangalizi wa maadabara.

Dr Nevio Zagara ambaye ni mwakilishi wa WHO Yemen amesema , jitihada za WHO kupeleka vifaa za matibabu Yemen, ni hatua nzuri katika kuziwezesha hospital za Yemen ambazo zimelemewa na wagonjwa wengi lakini huduma hazitoshelezi kutokana na uwezo mdogo wa kuwahudumia wagonjwa.

Aidha Dr Nevio amesema japo hali ya usalama ni hatarishi kwa watoa huduma wa WHO na mashirika  mengine ya kimataifa,  bado WHO ina wajibu wakusaidia  huduma za afya nchi nzima  ili kuokoa maisha ya mamiolini ya wananchi wasio na hatia .