Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Wakazi wa Kaya, Burkina Faso wakipokea mgao wa chakula.
WFP/Mahamady Ouedraogo

Heko Burkina Faso kwa kuweka mazingira bora ya mchakato wa kuelekea uchaguzi mkuu Kesho:Guterres

Katika mkesha wa kuamkia uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge nchini Burkina Faso hapo kesho Jumapili Novemba 22, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameipongeza serikali, viongozi wa kisiasa na watu wa Burkina Faso kwa kudumisha mazingira ya kuheshimiana katika wakati wote wa mchakato wa uchaguzi licha ya changamoto lukuki zinazolikabili taifa hilo la Afrika Magharibi.

Watoto wakimizi wakionesha kuunga kwao mkono shughuli za shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR za kutokomeza usafirishaji haramu huko Wad Sharige Mashariki mwa Sudan.
© UNHCR/Osama Idriss

Simulizi Yangu: Kukabili usafirishaji haramu Malawi

Maxwell Matewere, mtaalamu katika ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuzuia uhalifu na madawa ya kulevya, (UNODC) nchini Malawi, amekuwa akiendelea na harakati zake za kukabiliana na usafirishaji haramu wa binadamu kwa zaidi ya miongo miwili. Leo hii anapatia mafunzo maafisa mbali mbali nchini Malawi kuzuia na kukabili uhalifu: mwaka huu pekee licha ya janga la Corona au COVID-19, ameweza kuokoa watu 300 waliokuwa wakumbwa na usafirishaji haramu sambamba na kukamata watu 31 wahusika wa uhalifu huo.