Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Watoto wakimizi wakionesha kuunga kwao mkono shughuli za shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR za kutokomeza usafirishaji haramu huko Wad Sharige Mashariki mwa Sudan.

Simulizi Yangu: Kukabili usafirishaji haramu Malawi

© UNHCR/Osama Idriss
Watoto wakimizi wakionesha kuunga kwao mkono shughuli za shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR za kutokomeza usafirishaji haramu huko Wad Sharige Mashariki mwa Sudan.

Simulizi Yangu: Kukabili usafirishaji haramu Malawi

Haki za binadamu

Maxwell Matewere, mtaalamu katika ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuzuia uhalifu na madawa ya kulevya, (UNODC) nchini Malawi, amekuwa akiendelea na harakati zake za kukabiliana na usafirishaji haramu wa binadamu kwa zaidi ya miongo miwili. Leo hii anapatia mafunzo maafisa mbali mbali nchini Malawi kuzuia na kukabili uhalifu: mwaka huu pekee licha ya janga la Corona au COVID-19, ameweza kuokoa watu 300 waliokuwa wakumbwa na usafirishaji haramu sambamba na kukamata watu 31 wahusika wa uhalifu huo.

 

Nilikuwa kijana, na ndio kwanza nimehitimu shahada ya kwanza ya sheria, pindi nilipokumbana na janga la usafirishaji haramu. Ilikuwa mwaka 1998 nilikuwa nafanya kazina shirika la kiraia nikihudhuria warsha nchini Afrika Kusini.

Dereva wa teksi alinieleza kuhusu wasichana wawili kutoka nchini mwangu ambao walikuwa wanafanya kazi kwenye baa moja mjini Johannesburg. Alisema kuwa alikuwa ana hofu kubwa sana juu yao.

Wasichana hao walikuwa ni ndugu wakiwa na umri wa miaka 14 na 16. Nilikutana nao na kubaini kuwa walikuwa wamesafirishwa kiharamu kutoka Malawi hadi Afrika Kusini wakitumikishwa kwenye ukahaba. Walikuwa katika hali mbayá mno kimwili na kiakili.

Niliweza kupanga safari yao ya kurejea Malawi. Leo, mmoja wao anafanya kazi ya uhasibu na mwingine ni mwalimu katika shule ya msingi. Bado tunaendelea kuwasiliana na mimi kwao ni kama baba yao.

Tukio hili lilinitia moyo kujikita katika kazi ya kukabiliana an usafirishaji haramu,na baada ya Malawi kuridhia itifaki ya mkataba wa Umoja wa Mataifa wa kudhibiti usafirishaji haramu wa binadamu wa mwaka 2005, nikawa mjumbe wa kamisheni ambayo ilitunga sheria ya kwanza ya kitaifa ya kukabili usafirishaji haramu wa binadamu. Sheria hiyo Ilianza kutumika mwaka 2015.

Maxwell Matewere 9kushoto) mtaalamu wa kuzuia uhalifu UNODC Malawi, akiwa na maafisa wawili wakati wa uchunguzi wa usafirishaji haramu Malawi.
UNODC
Maxwell Matewere 9kushoto) mtaalamu wa kuzuia uhalifu UNODC Malawi, akiwa na maafisa wawili wakati wa uchunguzi wa usafirishaji haramu Malawi.

Mamia wanasafirishwa kiharamu kila mwaka

Usafirishaji haramu wa binadamu ni tatizo kubwa nchini mwangu, lakini kwa wakati huo, hakukuwepo na uelewa wa kutosha kuhusu uhalifu huu. Kila mwaka mamia ya wanawake, wanaume na watoto wengi wao kutoka maeneo ya vijijini, husafirishwa kiharamu ndani na nje ya nchi wakitumikishwa kwenye kazi pamoja na ukahaba.

Lakini leo hii, nchi yangu ina mbinu za kisheria za kushtaki wasafirishaji haram una kuwapatia ulinzi manusura. Hii ni hatua kubwa sana. Ni kazi yangu kusaidia utekelezaji wa sheria za kimataifa na kitaifa pamoja na mpango wa kitaifa ulioandaliwa na hufanyiwa marekebisho kila wakati kwa msaada wa UNDOC.

Nasafiri maeneo mbali mbali ya nchi, kufundisha, kujengea uwezo na kuwapatia ujuzi maafisa wa kusimamia sheria ambao wanahusika na kesi za usafirishaji haramu wa binadamu. Nawaelezea jinsi wanaweza kutumia sheria kubaini kesi, kutambua na kulinda manusura na hatimaya kufungulia mashtaka wahalifu.

Maxwell Matewere akizungumza na jamii nchini malawi kuhusu madhara ya usafirishaji haramu wa binadamu.
UNODC
Maxwell Matewere akizungumza na jamii nchini malawi kuhusu madhara ya usafirishaji haramu wa binadamu.

Maafisa wanaohusika na kesi za usafirishaji haramu—maafisa polisi, maafisa wafuatiliaji mipakani, na wachunguzi, wanahamasishwa kupatia kipaumbele haki na mahitaji ya manusura, na huwa ninafanya kazi na maafisa ustawi wa jamii ambao husaidia manusura katika safari yao ya kukwamuka kutoka machungu wanayokuwa wamepitia ikiwemo pia kuwa nao karibu wanapokuwa wanatoa ushahidi kwenye kesi mahakamani.

Natembelea maeneo ya vijijini, ambako nazungumza na viongozi wa kijadi wa vijiji kuhusu usafirishaji haramu na mbinu zinazotumiwa na wasafirishaji: watu hawa wana ushawishi mkubwa kwenye jamii zao katika kubadili tabia. Natembelea pia shule, vituo vya afya na makanisa kuelimisha kuhusu uhalifu huo. Ni jambo linalonipatia faraja kufanya kazi na Umoja wa Mataifa na kupata mlishonyuma kutoka kwa washiriki wa mafunzo ninayotoa.

Kuangazia mwanga kwenye uhalifu uliofichika

Naona ufanisi wa kazi yangu, kupitia idadi kubwa ya watu wanaookolewa kutoka kwa wasafirishaji haramu. Idadi pia ya wanaokamatwa na kesi ambazo zinafunguliwa na wahusika kuhukumiwa.

Kuna kesi kadhaa ambazo nimehusika na ambazo ninajivunia. Miongoni mwao ni ile ya kunusuru wamalawi waliokuwa wakitumikishwa huko Kuwait na Iraq na hatimaye wakarejea nyumbani salama. Halikadhalika, tulinusuru raia wa Nepal ambao hivi karibuni walikuwa wamesafirishwa kiharamu hadi Malawi.

Pia kufuatia mafunzo niliyotoa msimu wa kiangazi mwaka huu, kuna watoto walinusuriwa kutoka ndoa za lazima. 

Baadhi ya kesi nilizoshughulikiwa zinatumiwa na mawakili na waendesha mashtaka. Halikadhalika polisi wa Malawi wanatumia kwenye mafunzo yao kwa makuruta wapya.

Katika nchi yangu na kimataifa, ninatambuliwa kama shujaa. Mapema mwaka huu, nilitunukiwa tuzo na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani. Lakini kwangu mimi, tuzo bora zaidi ni kuona jinsi kazi yangu inaangazia kitaifa, kikanda na kimataifa suala la usafirishaji haramu binadamu, ambalo ni janga lililofichika.

Tunahitaji Maxwell wengi zaidi Malawi

Watunga sera wanatambua kuwa usafirishaji haramu wa binadamu ni jambo linalotia hofu kila uchao na linahitaij kushughulikiwa. Nchini Malawi hivi sasa vyombo vya habari vinatekeleza jukumu muhimu la kuangazia janga hili. Naona kuwa ni wajibu wangu kuhakikisha kuwa hakuna Maxwell mmoja tu, lakini Maxwell wengi zaidi. Nataka kufundisha watu wengi ili nchi yangu iweze kushughulikia kwa ufanisi tatizo hili.

Manusura wa usafirishaji haramu nchini Mauritania
© Sibylle Desjardins / IOM
Manusura wa usafirishaji haramu nchini Mauritania

Kupitia kazi yangu, naweza kuleta tofauti na kusimama kidete kwa ajili ya watu walio hatarini na kuzuia usafirishaji haramu. Hiki ni kitu kinanitia moyo na hamu ya kuendelea kusaidia wahanga, kwa kuwa machungu yao yananitia hofu kubwa.

Wakati mwingine kazi yangu inanigusa kihisia. Ninaona vitu vibaya, nahoji kwa nini watu wanatekeleza uhalifu huu hasa kwa watoto wasio na hatia. Lakini naweza kuweka mizania kati ya maisha yangu binafsi na ya kikazi.
Nina watoto watatu, mvulana mwenye umri wa miaka 13, na wasichana wawili mmoja miaka 7 mwingine 4.

Ninapokuwa nyumbani, natumia muda mwingi nao. Mwishoni mwa wiki, tunakwenda kanisani. Mke wangu na wanangu huwa wananikosa sana ninaposafiri. Watoto wangu wakubwa wawili wanafahamu kuhusu kazi yangu, lakini huwa mjadala sana wa kina na wao kuhusu kazi hiyo.

Mtoto wangu wa kike mwenye umri wa miaka 7 hivi karibuni aliulizwa shuleni apeleke picha ya mtu mashuhuri, na alichukua picha yang una kuelezea darasa lake kuwa baba yake ni shujaa kutokana na kazi anayofanya.
TAGS: Malawi, Usafirishaji Haramu, Maxwell Matewere, UNODC